KWA WAHARIRI WOTE
Wakubwa Wahariri
Naungana nayi katika kuumaliza vizuri Mwaka 2013. Aidha, nachukua nafasi hii kuwatakia Heri nyingi za Mwaka 2014. Uwe ni mwaka wa Baraka na Mafanikio kwetu sote. Napenda pia kuwapongezeni nyote kwa detailed reporting ya shughuli ya jana ya Kukabidhiwa kwa Ripoti (which includes Rasimu ya Katiba) ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa Mheshimiwa Rais Kikwete na Mheshimiwa Rais Ali M. Shein. Ni kazi nzuri – well done!
Jambo moja tu la msingi ambalo Mheshimiwa Rais Kikwete alilisisitiza jana ni kwamba there already appears some sections of the Press ambazo tayari zimeanza kupotosha shughuli nzima ya jana kwa kuielezea Ripoti ya jana kuwa ni Katiba Mpya.
Naamini kuwa kila mmoja wetu anajua kuwa Ripoti ya Tume ambayo inashirikisha Rasimu ya Katiba, siyo Katiba Mpya. Mchakato wa kupata Katiba Mpya ndio kwanza umeingia katika hatua nyingine, hatua muhimu sana. Ripoti ya Tume, ikiwa ni pamoja na Rasimu ya Katiba, lazima viende sasa kujadiliwa katika Bunge la Katiba.
Na hata baada ya kujadiliwa na Bunge la Katiba na Wabunge wa Bunge hilo kufikia maamuzi, ni kwamba maamuzi hayo lazima yaende kwa wananchi kwa ajili ya Kura ya Maoni – Referendum. Ni sisi wananchi ambao tutaamua, Kwa sasa tunaendelea kutumia Katiba ya sasa na hakuna Katiba Mpya. Natumai kuwa tuzingatie ukweli huu wakati tunaendelea kuandika na kutangaza habari za jambo hilo kubwa na la kihistoria katika nchi yetu.
Once again – A Happy and Prosperous New Year to us all.
SALVA RWEYEMAMU, MKURUGENZI WA MAWASILIANO
IKULU, DAR ES SALAAM. 31 DESEMBA, 2013