WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamisi Kagasheki amejiuzulu muda huu bungeni mjini Dodoma. Balozi Kagasheki ametangaza kujiuzulu baada ya Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira kuibua hali ya ukiukwaji wa haki za binadamu uliofanya na Oparesheni Maalumu ya Tokomeza ujangili iliyosimamiwa kwa kiasi kikubwa na Wizara yake.
Kagasheki ametangaza kujiuzulu muda mfupi baada ya kupewa nafasi ya kuzungumza kuchangia taarifa ya Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira iliyobaini mauaji, mateso, dhuluma, udhalilishaji na uonevu mkubwa uliofanyika kwa baadhi ya wananchi waliokumbwa na operesheni hiyo.
“Lengo la operesheni hii lilikuwa jema lakini yametokea yalio tokea…mimi ni mtu mzima nimesikia yaliyosemwa,…nime-resign (nimejiuzulu), nitachukua hatua zinazostahili ili kuzialifu mamlaka husika,” alisema Balozi Kagasheki na kumaliza. Taarifa zaidi ya habari hii baadaye kidogo…!