Uganda Sasa Mashoga, Wasagaji Kufungwa Maisha
BUNGE la nchini Uganda limepitisha mswaada utakaowabada watakao tiwa hatiani kushiriki mapenzi ya jinsia moja kuwa sheria. Mswaada huo unangojewa kuwa sheria kamili baada ya Rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni kuutia saini.
Mswaada huo wa kupinga mapenzi ya jinsia moja na usagaji ulipitishwa na bunge hivi karibuni na inasemekana kuwa mtu yeyote atakaye kuwa na taarifa za watu wanaofanya vitendo hivyo na kushindwa kutoa taarifa kwa vyombo vya sheria naye ataingia hatiani.
Pia bunge hilo liliidhinisha mswaada unaopiga marufuku maonesho ya picha za chafu. Mswada huo unaharamisha kitu chochote kitakachoonyesha sehemu nyeti kama vile matiti, mapaja, makalio au tabia yoyote inayozua uchu wa mapenzi.
Kulingana na mswada huo, sheria iliyopo sasa kuhusu picha chafu haihusu zaidi picha hizo bali linahusu uchapishaji ,mawasiliano, taarifa , burudani, maonyesho katika kumbi za kuigizia, miziki inyochezwa katika vyombo vya habari, densi, sanaa, mitindo na picha za runinga.
Mapema mwaka huu Waziri wa maadili wa Uganda, Simon Lokodo, alipendekeza kuwa mwanamke yeyote anayevalia nguo ambayo inafika juu ya magoti anatakiwa kukamtwa na kuadhibiwa kisheria. Mswada huo unangoja kuidhinishwa na rais kabla ya kufanywa kuwa sheria kamili.
Uganda ni nchi inayoshikilia mawazo ya kihafidhina yaani isiyopendelea mageuzi katika mawazo na inaandaa sheria ya kuwaadhibu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja ikijumuisha hukumu ya kifo katika baadhi ya kesi.