Wanafunzi Waongoza Kunyakua Zawadi za Pambika na Samsung Droo ya Tano
JUMLA ya wanafunzi watano toka mikoa ya Mwanza, Dodoma, Kilimanjaro, Dar es Salaam na Morogoro wameibuka washindi kati ya washindi 15 wa droo ya tano ya promosheni ya Pambika na Samsung na kuzawadiwa zawadi mbalimbali kutoka Samsung.
Kutoka Mwanza Adam Kennedy (18) mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Alpha alishinda deki ya DVD toka Samsung, Kiza Shija (22) mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mt. John, Dodoma mshindi wa Muziki wa Nyumbani, Ezekiel Brown (34) mwanafunzi chuo cha kodi toka Kilimanjaro ambae ameshinda Jiko la Kupashia chakula, Emmanuel Issaya (38) mkazi wa Dar es salaam ambae ni mshindi wa deki ya DVD na Wilfred Tembo (45) mwanafunzi Chuo cha Utumishi kutoka Morogoro ambae ni mshindi wa kompyuta mpakato.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa baadhi ya washindi wa Pambika na Samsung droo ya tano, Meneja Mauzo na Usambazaji wa Samsung Tanzania Bw. Sylvester Manyara alisema kwamba promosheni ya Pambika na Samsung imetoa washindi toka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania tangu kuanza kwake huku idadi ya watu wanaosajili bidhaa zao baada ya kununua ikiongezeka kwa zaidi ya asilimia 30.
“Tumepata washindi toka mikoa mbalimbali ya Tanzania na ni jambo la furaha kwetu kwamba bidhaa za Samsung zina mchango mkubwa katika maisha ya watu wengi Tanzania nzima. Samsung inafuraha kuona washindi wengi kupitia promosheni hii ya Pambika na Samsung wakibadili maisha yao kupitia bidhaa zetu halisi”, alisema Bw. Manyara
“Tumepata ongezeko la zaidi ya asilimia 30 kwa wateja kusajili bidhaa zao mara wanaponunu na hii inatupa faraja zaidi kwa lengo letu la kuhamasisha matumizi ya bidhaa halisi linafanikiwa. Promosheni za Pambika na Samsung imekuwa wazi toka kuanza kwake huku ikifuata taratibu zote chini ya usimamizi wa karibu toka Bodi Michezo ya Kubahatisha Tanzania, tumebakisha siku chache kabla ya kutoa zawadi kubwa ya gari jipya aina ya Mitsubishi Double Cabin Jumatatu ya wiki ijayo ambapo mteja mmoja mwenye bahati atajishindia. Bado natoa wito kwa watanzania wote kununua bidhaa halisi za Samsung na kuzisajili ili kuingia kwenye droo” aliongezea Bw Manyara.
Akizungumza toka Dodoma kwa njia ya simu, Bi Kiza Shija, mshindi wa Muziki wa Nyumbani alisema kwamba zawadi aliyopata toka Samsung ni zawadi ya sikukuu za Kristmas na Mwaka Mpya na itanisaidia sana kuweza kupumzika kwa kusikiliza muziki baada ya masomo “Sikuwa najua kama nimeingia kwenye droo yya Pambika na Samsung japo kuwa nilisajili simu yangu katika mfumo wa e-warranty” alisema Bi. Kija Shija mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mt. John cha Dodoma.
Bi. Kiza aliongeza kwamba “Kwanza nilipoteza simu yangu siku mbili tu baada ya kuinunua katika duka la Samsung hapa Dodoma, pili sikuwa na imani sana na michezo ya kubahatisha na wala matangazo yake huwa siyafuatilii. Nilikuwa nimeshtuka baada ya kupokea simu Jumatatu na kuniambia nimeshinda Muziki wa nyumbani toka Samsung baada ya kununua simu halisi ya Samsung na kuisajili, asante sana Samsung kwa zawadi hii ya Kristmas na Mwaka mpya, kidogo machungu ya kupoteza simu yamepungua”
Washindi wengine wa droo ya tano walikuwa ni Docus Moses (22) Mbeya, Sophia Abel (50) Dar es Salaam, Tumaini Luca (28) Morogoro, na Zoheri Mohamed Hussein (49) Dar es salaam washindi wa deki za DVD kila mmoja. Shamasha Said (27) Arusha, na Joel Mlaki (25) Dar es Salaam walijishindia Muziki wa nyumani kila mmoja.
Wengine ni Mustafa Turbal (23) toka Dar es Salaam mshindi wa Mashine ya kufulia nguo na Abbas Murtaza (32) mshidni wa luninga ya LED 32’. Collins Nyakunga (35) Dodoma, Victoria Morungu (30) Dar es Salaam walijishindia jiko la kupashia chakula kila mmoja..
Kuingia kwenye droo na kujihakikishia nafasi ya kushinda, mteja atatakiwa kununua simu yoyote halisi ya Samsung na kuisajiili katika mfumo wa dhamana ya ziada kwa kutuma nambari za utambulisho wa simu hiyo yaani namba za “IMEI” kwenda 15685, na kwa wale watakaonunua bidhaa nyengine watatakiwa kujaza fomu maalum zinazopatikana katika maduka yote ya Samsung ambapo wataingia kwenye droo na kuwa na nafasi ya kushinda zawadi kubwa ya Mitsubishi Double Cabin katika droo ya mwisho itakayofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam siku ya Jumatatu ya Desemba 23, 2013.