Pichani juu ni baadhi ya wasanii chipukizi watakaopewa nafasi ya kuonesha vipaji vyao Jumamosi hii katika tamasha la kukuza vipaji vya sanaa na muziki litakalofanyika viwanja vya Biafra Kinondoni jijini Dar es Salaam Dec 14. Wasanii hawa wataungana na wasanii wengine vijana walionza kufanikiwa katika tasnia akiwemo msanii Ally Nipishe na kuonesha vipaji vyao kwa vijana wenzao.
Baadhi ya wasanii chipukizi watakaoonesha vipaji vyao wakiwa na msaanii anayeanza kufanya vizuri katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya Ally Nipishe (watatu kutoka kulia waliosimama) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufanya mazoezi na kubadilishana uzoefu.
Msanii Ally Nipishe (aliyevaa kofia) akitoa ushauri kwa baadhi ya vijana waliopewa nafasi kutumbuiza katika tamasha la vipaji vya Sanaa na Muziki kwa vijana lililoandaliwa na UCA-Tz kwa kushirikiana na kampuni za Zantel, Coca Cola- Tanzania, Maezeki, LBGY Media na mtandao wa dev.kisakuzi.com.
Mmoja wa wasanii chipukizi (wa kwanza kulia) akipokea mrejesho baada ya kuimba wimbo wake toka kwa wadau vijana wa UCA Tz leo. Wa kwanza kushoto ni MC wa zoezi la kuwatambua chipukizi waliopata nafasi ya kutumbuiza kwenye tamasha hilo.
Baadhi ya vijana wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiendelea kutoka kwa vijana waandaaji wa UCA-Tz leo.
Mwanadada mwakilishi wa Vijana kutoka UCA-Uganda aliyewasili Tanzania kushiriki tamasha hilo akitoa mchango wake kwa wasanii vijana walioshiriki kwenye zoezi hilo.
Baadhi ya vijana waandaaji wa Tamasha la Vipaji kwa Sanaa na Muziki kwa Vijana UCA TZ wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kikao cha majadiliano namna ya kufanikisha tamasha hilo litakalozinduliwa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.