Kocha mkuu Simba kutua Dar

KOCHA mkuu wa timu ya soka ya Simba, Mganda Mosses Bassena atarajiwa kuingia nchini kukinoa kikosi kwa ajili ya Simba Day na mchezo wa ngao ya hisani dhidi ya wahasimu wao Yanga Agosti13.

Bassena alikuwa nchini kwao Uganda kwa ajili ya mapunziko mafupi baada ya kumalizika kwa mashindano ya Kombe la Kagame yaliomalizika hivi karibuni na Simba kukubali kichapo cha 1-0 dhidi ya Yanga.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii Dar es Salaam jana Ofisa Habari wa Simba Ezekiel Kamwanga, alisema wamejiandaa vizuri kishiliki mashindano hayo.

“Tunamsubili kocha Bassena ambaye yuko mapumzikoni na tinatarajia atarudi kesho au kesho kutwa ili timu yetu iingie rasmi kambini kwa ajili kukinoa kikosi kwa ajili ya mashindano hayo pamoja na ligi kuu msimu ujao” alisema Kamwanga.

Alisema mpaka sasa maadalizi ya timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya soka Tanzania bara yanaenda hivyo wanatarajia kufanya vizuri katika mashindano hayo.

Kwa mujibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania TFF, Simba imewaacha Musa Hassan ‘Mgosi’, Juma Jabu na Mohammed Banka katika kikosi kitakachonolewa kwa ajili ya Ligi Kuu Msimu ujao.

Wakati huo huo, mabingwa wa soka wa Afrika Mashariki na Kati Yanga wanatarajia kuingia kambini leo kwa ajili ya mchezo wa Ngao Hisani utakaofanyika kwenye uwanja wa Taifa Agosti 13.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Yanga Louis Sendeu alisema timu iko tayari na utaanza mazoezi kwa ajili ya mchezo huo.

“Tunaanza mazoezi tarehe 19 na wachezaji wako tayari hivyo Simba wasubili kichapo kingine zaidi ya walichokupata kwenye fainali za Kagame” alisema Sendeu