BONDIA Fransic Miyeyusho wa Tanzania amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi katika mchezo wake na David Chalanga kutoka Kenya utakaofanyika Desemba 31 katika ukumbi wa Msasani Klabu. Mchezo huo wa kufunga na kuukaribisha mwaka utakuwa wa raundi nane.
Akizungumzia mpambano huo bondia Miyeyusho alisema yupo fiti wakati wowote kupambana na mpinzani wake hata kama ingeamuliwa pambano hilo lifanyike leo. “Mimi nipo tayari muda wote kupambana…,” alisema Miyeyusho.
Pamoja na hayo mchezo huo ni chachu kwa mabondia wote wawili ambao wanatamba Afrika Mashariki kwa kushindsnis mikanda mikubwa ya ubingwa na kujijengea rekodi ya ushindi.
Hata hivyo kabla ya mpambano huo mkubwa kutakuwa na mapambano ya utangulizi, ambapo bondia Iddy Mnyeke ataoneshana ubabe na Cosmasi Cheka, Antony Mathias akizipiga na Fadhili Majiha, huku Ibrahimu Class ‘King Class Mawe’ akizichapa na Mohamed Kashinde.