Na Mwandishi Wetu
RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameunda kamati mbili maalumu (ad hoc) kwa ajili ya kutathmini muundo wa ligi na kupendekeza namna ya kuuboresha, na kutahmini muundo wa Bodi ya Ligi na kupendekeza namna ya kuuboresha ikiwemo kuunda kampuni.
Kamati ya Kutathmini Muundo wa Ligi inaongozwa na Kocha wa zamani wa Taifa Stars, Dk. Mshindo Msolla wakati Katibu ni Ofisa Mashindano wa TFF, Idd Mshangama. Wajumbe ni Rahim Kangezi, Amri Said, Sunday Manara, Salim Bawazir na Lucas Kisasa.
David Nchimbi kutoka Delloitte ndiye anayeongoza Kamati ya Muundo wa Bodi ya Ligi wakati wajumbe ni Edwin Kidifu (Mwanasheria wa SUMATRA), Jones Paul (Mkurugenzi wa Sunderland/Symbion Academy), Evans Aveva, John Jambele, Masoud Sanani na Pelegrinius Rutahyuga.
Wakati huo huo, Rais Malinzi amemteua Pelegrinius Rutahyuga kuwa Mshauri wa Rais (Ufundi). Mshauri wa Rais (Utawala) atateuliwa baadaye.
AFRIKA KUSINI KUTUA KWA SOUTH AFRICA AIRWAYS
Wakati huo huo; Kikosi cha Afrika Kusini (Basetsana) kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kwa wasichana wenye umri chini ya miaka 20 dhidi ya Tanzania (Tanzanite) kinatua nchini kesho (Desemba 5 mwaka huu).
Afrika Kusini itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) itatua saa 8 kamili mchana kwa ndege ya South Africa Airways.
Wanaounda Basetsana ni makipa Kaylin Swart, Regirl Ngobeni na Juliet Sethole. Mabeki ni Abongile Dlani, Caryn van Reyneveld, Chamelle Wiltshire, Meagan Newman, Nomonde Nomthseke, Tiisetso Makhubela na Vuyo Mkhabela.
Viungo wapo Amanda November, Amogelang Motau, Gabriella Salgado, Koketso Mamabolo, Nomvula Kgoale na Thembi Kgatlane. Washambuliaji ni Mosili Makhoali, obyn Moodaly, Sduduzo Dlamini na Shiwe Nogwanya.
Viingilio katika mechi hiyo itakayochezwa Jumamosi (Desemba 7 mwaka huu) ni sh. 1,000 kwa viti vya rangi ya kijani, bluu na orange, sh. 2,000 kwa VIP C, sh. 5,000 kwa VIP B wakati VIP A watalipa sh. 10,000.