KATIBU wa Chama cha Walimu wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, Bw. Adagoti Komba Daudi ameibuka mmoja ya washindi 15 wenye bahati katika droo ya tatu ya promosheni kabambe ya Pambika na Samsung na kuzawadiwa deki mpya ya DVD kutoka Samsung. Komba alikuwa ni Mmoja ya washindi hao waliopatikana katika droo ya kila wiki ya Pambika na Samsung ambapo promosheni hiyo itakayodumu kwa wiki sita sasa imefikia wiki ya tatu na watu 45 kutoka mikoa mbalimbali wameshajishindia bidhaa mbalimbali.
“Nilipokea simu ambayo sikuitarajia Jumatatu asubuhi kutoka kwenye namba ambayo siifahamu iliyoanza kuniuliza maswali mengi baada ya kujitambulisha, sikuwa najiamini mwanzoni kutokana na hayo maswali kabla ya mtu huyo aliyejitambulisha kutoka Samsung kuniambia kwamba mimi ni mshindi wa deki mpya ya DVD kupitia promosheni inayoendelea ya Pambika na Samsung” alisema Bw. Komba katika mahojiano
“Kwakweli ilikuwa ngumu kukubali kile nilichokuwa nakisikia kutoka kwa huyo mtu, unajua dunia imebadilika na matapeli siku hizi wapo kila kona ambao wanatumia mbinu mbalimbali kujipatia chakula chao cha kila siku kwa hiyo nilidhani kuna mtu ananitania au alitaka kunitapeli. Ninawashukuru sana Samsung kwa hii zawadi, Pambika na Samsung sio tu inatoa zawadi kwa wateja lakini pia inaleta imani juu ya ubora wa bidhaa zao” alimalizia Komba
Washindi wengine ambao wamepata zawadi ya deki ya DVD kila mmoja ni Issa Richard Moshi (23) mchimbaji madini kutoka moshi, Agnes John Mkalango (30) wakala wa Mpesa toka Dar es salaam, Kelvin Walter Nkya (29) Ofisa Kodi na Mfanyabiashara Abdallah Mohamed-Ally Gilamaly (50) wote kutoka Dar es salaam.
Bernadeta Peter Magayane (44) mkazi wa Dar es salaam amejinyakulia jokofu lenye dhamana ya miaka kumi toka Samsung wakati kompyuta mpakato mpya ilikwenda kwa mkazi wa Dar es salaam Bw. Hamad Abdallah Hemed (43). Askari wa Jeshi la Polisi kutoka mkoani Dodoma Antonia Julius Masele (45) alijinyakulia Luninga mpya ya LED ya inchi 32 toka Samsung
Mbeya, Arusha na Dar es Salaam ilitoa washindi wanne waliojishindia ‘Home Theatre’ kila mmoja, Abdallah Said Ndeke (41) ambae ni mfanyabiahsra na Veronica Gunju wote wakazi wa Dar es salaam wakati kutoka Mbeya ni Faustine K. Kirusya (45) na kutoka Arusha ni Praygod Amos (39). Washindi wengine ni Hillary Henry Nkindi (27) wa Dodoma, Aloyce Simba Maira (41) na Stella John Brand (26) toka Dar es salaam kila mmoja amejinyakulia jiko la kupashia chakula
Meneja Mauzo na Usambazaji toka Samsung Tanzaia, Bw. Sylvester Manyara akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi iliyofanyika Quality Center, Dar e salaam alisema kwamba “Tumezindua Pambika na Samsung ili kuongeza ufahamu wa bidhaa halisi na kuongeza kasi ya mapambano dhini ya bidhaa feki, kampeni hii ya kitaifa inafanyika kwa bidhaa zote za Samsung. Tukiwa na mfumo wa e-warranty, Samsung inatoa fursa kwa wateja kujua uhalisia wa bidhaa wanazonunua”
“Hii ni huduma nyengine toka Samsung ili kutetea haki za wateja na kusaidia kulinda bidhaa wanazonunua, pia kuwalinda kutokana na kununua bidhaa feki au kutafuta bidhaa iliyoibiwa au kupotea. Hivyo kampeni hii inawazawadia wale wanaonunua bidhaa halisi na kuzisajili kwenye huduma hii kila wiki” alimalizia Bw. Manyara.
Kuingia kwenye mchakato wa kushinda, mteja atatakiwa kununua simu yoyote halisi ya Samsung na kuisajili kwenye huduma Maalum ya ‘E-Warranty’ kwa kutuma namba 15 za utambulisho wa simu yake yaani ‘IMEI’ kwenda namba 15685. Na kwa yule atakaenunua bidhaa nyingine ya Samsung anatakiwa kujaza fomu Maalum inayopatikana katika maduka yote ya Samsung na kwa mawakala waliosajiliwa waliopo nchi nzima na kujihakikishia nafasi ya kushinda katika droo za kila wiki na ile ya mwisho.