Bremen, Ujerumani
BENDI maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU ughaibuni, usiku tarehe 23 Novemba 2013 walifanikiwa kwa mara nyingine tena kuliteka jiji la Bremen, kule ujerumani. Kiongozi wa bendi hiyo kamanda Ras Makunja wa FFU alikiongoza jukwaani kikosi kazi chake katika jumba la Übersee-Museum akiwa na matumaini kuwa wanaenda kumbuiza washabiki high class wenye adhi ya kibwanyenye lakini mziki ulipoanza mdundo uliwachanganya washabiki na kuwadatisha akili! Kila mmoja alijimwaga uwanjani!
Ngoma Africa Band walijikuta wapo katika kibarua kama kawaida yao cha kushambulia kwa virungu vya muziki na kufanikiwa kuutapanua uwigo wake kwa kuwanasa washabiki wengi wa kimataifa. Bendi hiyo maarufu iliyojiimarisha na kujenga himaya ya kimataifa kwa kutumia muziki wake.
Imeshatajwa mara nyingi kuwa bendi bora ya kiafrika barani ulaya, bendi ya Ngoma Africa inafanananishwa sawa na kikosi maalumu cha kuzuwia ghasia FFU, pia ina majina mengi ya utani na kiusanii kama vile viumbe wa ajabu “Anunnaki Elien” n.k ambayo imepewa na washabiki au wapenzi wake, kiongozi wake pia ana majina kama vile kamanda Ras Makunja wa FFU, mtawala wa Anunnaki Empire. Ngoma Africa band wanasikika at www.ngoma-africa.com