Pambika na Samsung Yaendelea na Jitihada za Kuboresha Maisha ya Watanzania

Mratibu wa promosheni ya Pambika na Samsung Bw. Lawrence Andrew akiongea na moja ya washindi wa promosheni ya Pambika na Samsung. Washindi wa droo ya pili waliopatikana na zawadi zao ni Johnson Choi (54) Muziki wa nyumbani - mkazi wa Arusha, Robert David Maye (39) Jokofu – mkazi Dsm, Erakissa Siginda (38) Samsung Galaxy Tab 10.1 – Mkazi wa Dsm, Laurent Madafu (26) Luninga ya LED Mkazi wa Arusha, Hemed Rashid Hemed (25) Deki ya DVD – Mkazi wa Dsm, Martin H. Mwashambwa (35) Jiko la kupashia chakula – Mkazi wa Dsm, Jamari Omary Marwa (34) Jiko la Kupashia Chakula, Abdallah Idd Ally wa Arusha (26) Mshindi wa deki ya DVD.

Mratibu wa promosheni ya Pambika na Samsung Bw. Lawrence Andrew akiongea na moja ya washindi wa promosheni ya Pambika na Samsung. Washindi wa droo ya pili waliopatikana na zawadi zao ni Johnson Choi (54) Muziki wa nyumbani – mkazi wa Arusha, Robert David Maye (39) Jokofu – mkazi Dsm, Erakissa Siginda (38) Samsung Galaxy Tab 10.1 – Mkazi wa Dsm, Laurent Madafu (26) Luninga ya LED Mkazi wa Arusha, Hemed Rashid Hemed (25) Deki ya DVD – Mkazi wa Dsm, Martin H. Mwashambwa (35) Jiko la kupashia chakula – Mkazi wa Dsm, Jamari Omary Marwa (34) Jiko la Kupashia Chakula, Abdallah Idd Ally wa Arusha (26) Mshindi wa deki ya DVD.

Mratibu wa promosheni ya Pambika na Samsung Bw. Larence Andrew akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa kuchezesha droo ya pili ya bahati nasibu ya Pambika na Samsung, jumla ya washindi 15 walipatikana ambao ni wa siku ya Jumatatu hadi Jumapili wiki iliyopita. Wengine pembeni ni Bw. Masenye Chacha, Meneja Uhasibu Samsung Tanzania na Kushoto ni Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Bw. Bakari Maggidy.

Mratibu wa promosheni ya Pambika na Samsung Bw. Larence Andrew akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa kuchezesha droo ya pili ya bahati nasibu ya Pambika na Samsung, jumla ya washindi 15 walipatikana ambao ni wa siku ya Jumatatu hadi Jumapili wiki iliyopita. Wengine pembeni ni Bw. Masenye Chacha, Meneja Uhasibu Samsung Tanzania na Kushoto ni Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Bw. Bakari Maggidy.

KATIKA kuhakikihsa inaendelea kuwazawadia wateja wa Samsung wanaonunua bidhaa halisi, promosheni ya Pambika na Samsung leo imefanya droo yake ya pili na kuendelea kuwapa furaha wateja wake 15 katika wiki ya pili ya promosheni hiyo.
“Muitikio wa wateja katika promosheni hii ya Pambika na Samsung inayoendelea ni wenye kutia moyo sana na Samsung bado tutaendelea na juhudi zetu katika kuyafanya maisha ya wateja wetu kuwa bora zaidi kwa kuwapa bidhaa zenye ubora zitakazokidhi hali halisi ya maisha ya kila mmoja” alisema Meneja Mauzo na Usambazaji, Samsung Tanzania Bw Sylvester Manyara wakati wa kufanyika kwa droo hiyo.
Katika wiki ya kwanza iliyofanyika Jumatatu ya wiki iliyopita, Pambika na Samsung ilipata washindi toka sehemu mbalimbali za nchi zikiwemo Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Tabora, Arusha, Dodoma, Moshi na Manyara ambapo wateja walijishindia bidhaa mbalimbali za Samsung kama Jokofu, Kompyuta mpakato, Jiko la umeme, Galaxy Tab 10.1, Luninga yenye LED inchi 32, muziki wa nyumbani na deki za DVD, ambapo droo hiyo ilifuatiwa na kukabidhi zawadi katika hafla fupi iliyofanyika Quality Center, jijini Dar esl Salaam.
“Pambika na Samsung bado inaendelea kuonyesha jukumu letu la kuwazawadia wateja wetu kwa mchango wao mkubwa kwenye bidhaa za Samsung. Tutaendelea kuwajali na kukamilisha ahadi zetu kwao kuhakikisha maisha ya wateja wetu kupitia bidhaa zetu bora yanakuwa rahisi na bora zaidi huku tukijali mchango wao wa kibiashara.” Aliongezea Bw Manyara.
Washindi wa droo ya pili waliopatikana na zawadi zao ni Johnson Choi (54) Muziki wa nyumbani – mkazi wa Arusha, Robert David Maye (39) Jokofu – mkazi Dsm, Erakissa Siginda (38) Samsung Galaxy Tab 10.1 – Mkazi wa Dsm, Laurent Madafu (26) Luninga ya LED Mkazi wa Arusha, Hemed Rashid Hemed (25) Deki ya DVD – Mkazi wa Dsm, Martin H. Mwashambwa (35) Jiko la kupashia chakula – Mkazi wa Dsm, Jamari Omary Marwa (34) Jiko la Kupashia Chakula, Abdallah Idd Ally wa Arusha (26) Mshindi wa deki ya DVD.

“Furaha iliyoonyeshwa na wateja wetu toka droo ya kwanza inatupa Faraja huku wateja wengi wakimiminika katika maduka ya Samsung kujipatia bidhaa halisi. Manunuzi ya bidhaa zetu halisi yameongezeka katika kila wiki tangu kuanza ka kampeni yetu hii. Ningependa kuwatakia kila la heri washindi wote na wale wote wanaoendelea kuinunua bidhaa zetu halisi na kujisajili katika huduma ya ‘E-Warranty’”. Alimalizia Bw Manyara
Ikizinduliwa Novemba 7, 2013 Pambika na Samsung ni promosheni ya wiki sita katika msimu huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka ikiwa na lengo la kupambana na bidhaa feki kama moja ya vikwazo kwa maendeleo ya Uchumi. Bidhaa feki za kielektroniki ambazo zinatishia uhai wa bidhaa halisi zinasababisha kushuka thamani kwa bidhaa halisi. Lakini pia kama hali ikiendelea kwa muda mrefu bidhaa hizo zitaathiri uzalishaji wa bidhaa halisi na kuongeza tatizo la ajira nchini.

Promosheni hii inalengo la kuwazawadia wateja ambao wananunua bidhaa halisi kuanzia simu mpaka bidhaa za nyumbani, bado ina wiki nne zaidi kabla ya zawadi ya mwisho ya gari aina ya Mitsubishi Double Cabin mpya kutolewa Desemba 23, 2013.

Kuingia kwenye mchakato wa kushinda, mteja atatakiwa kununua simu yoyote halisi ya Samsung na kuisajili kwenye huduma Maalum ya ‘E-Warranty’ kwa kutuma namba 15 za utambulisho wa simu yake yaani ‘IMEI’ kwenda namba 15685. Na kwa yule atakaenunua bidhaa nyingine ya Samsung anatakiwa kujaza fomu Maalum inayopatikana katika maduka yote ya Samsung na kwa mawakala waliosajiliwa waliopo nchi nzima na kujihakikishia nafasi ya kushinda katika droo za kila wiki na ile ya mwisho.
Kwa taarifa zaidi kuhusu Pambika na Samsung wasiliana na Bertha Ikua- Meneja Huduma kwa Wateja bertha@spearheadafrica.com au 0759 252 252