Pombe, Sigara na Vyakula Vyaongoza Kuleta Kisukari Tanzania

Mratibu wa Mradi wa Taifa wa Kisukari , John Gardner  akielezea jinsi wanavyofanya kazi ya kupunguza ugonjwa huo kwa kuhusisha sekta mbalimbali.

Mratibu wa Mradi wa Taifa wa Kisukari , John Gardner akielezea jinsi wanavyofanya kazi ya kupunguza ugonjwa huo kwa kuhusisha sekta mbalimbali.

Dk. Zakharia Ngoma)  wakati akitoa semina kwa waandishi wa habari kuhusu ugonjwa huo leo jijini Dar es Salaam.

Dk. Zakharia Ngoma) wakati akitoa semina kwa waandishi wa habari kuhusu ugonjwa huo leo jijini Dar es Salaam.

ASILIMIA 9.1 ya Watanzania wanaugua ugonjwa wa kisukari hali ambayo huchangia na unywaji wa pombe huvutaji wa sigara, ulaji wa vyakula usiofaa na kutokufanya mazoezi ya mwili. Hayo yamesemwa leo na Dk. Omary Ubuguyu kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) wakati akitoa semina kwa waandishi wea habari kuhusu ugonjwa huo leo jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo aliongeza kuwa asilimia ya idadi ya watu 80 hadi 90 wanaugua ugonjwa huo duniani.
“Unywaji wa pombe kuanzia chupa tano kwa wanaume na chupa 4 kwa wanawake huchangia kusababisha ugonjwa huu,” alisema Dk. Ubuguyu.

Kwa upande wake Mratibu wa semina hiyo, kutoka Mradi wa Taifa wa Kisukari, John Gardner alisema gharama ya matibabu ya ugonjwa huo ugharimu dola za Marekani milioni 378 ya asilimia 12 ya bajeti ya afya duniani kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2010, ambapo inaweza kufikia hadi zaidi dola milioni 400.

Akizungumzia kuhusu ugonjwa huo, Dk. Zakharia Ngoma alisema ulaji usiofaa na mtindo wa maisha huchangia kwa kiasi kikubwa. Hivyo hutumiaji wa vya kula vya asili , vya kuchemsha, mafuta, chumvi na sukari kidogo, mboga za majani kwa wingi na matunda kila siku, pamoja na vyakula vyenye virutubisho vyote husaidia kuepukana na ugonjwa huu,” alisema Dk. Ngoma.

Aliongeza kuwa hutumiaji wa vyakula vya jamii ya kunde na visivyokobolewa husaidia kuepuka ugonjwa huu, ikiwemo kunywa maji kwa wingi na kuepuka msongo wa mawazo.