Zitto Avuliwa Uongozi Ndani ya Chadema
TAARIFA ambazo zimetufikia hivi sasa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe amevuliwa nafasi zote za uongozi ndani ya Chadema. Zitto amevuliwa nafasi hizo za uongozi ndani ya Chadema baada ya kutuhumiwa kuandika taarifa za uchochezi kwenye mitandao ya kijamii.
Pia chama kimemuandikia barua kikimtaka ajitetee kwanini asifukuzwe ndani ya chama hicho. Habari zaidi zinafuata.