Wabunge nao watembelea maonyesho ya Wizara ya Nishati na Madini Dodoma!

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (CCM) akipata maelezo kutoka kwa mtaalamu wa mradi wa Biofueli Bi. Ester Mfugale mara alipotembelea banda la Wizara ya Nishati na Madini kwenye maonyesho yake yanayoendelea kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma.

Waziri Kivuli wa Wizara ya Nishati na Madini  Mhe.John Mnyika (CHADEMA) akimsikiliza kwa makini Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA) Bw. Paul Masanja mara alipotembelea banda hilo ili kupata maelezo juu ya shughuli za ukaguzi wa madini zinazofanywa na Wakala huo.
 

Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Gregory Teu, akipata maelezo kutoka kwa mtaalamu kutoka kampuni ya Arti Tanzania Limited inayofadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Bw. Abdalah Seushi  juu ya shughuli zinazofanywa na kampuni hiyo mara alipotembelea banda hilo kwenye maonyesho ya Wizara ya Nishati na Madini yanayoendelea katika viwanja vya bunge mjini Dodoma.

Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Gregory Teu, akipata maelezo kutoka kwa mtaalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Assa Mwakilembe juu ya shughuli zinazofanywa na Wizara hiyo mara alipotembelea banda hilo kwenye maonyesho yake yanayoendelea katika viwanja vya bunge Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Bw. David Jairo akipata maelezo ikiwa ni pamoja na kuonyeshwa juu ya shughuli za upimaji wa mafuta ya magari unavyofanywa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) mara alipotembelea banda hilo kwenye maonyesho ya Wizara ya Nishati na Madini yanayoendelea kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma. Anayetoa maelezo ni  Mhandisi Melania Kamugisha ambaye ni mtaalamu wa mamlaka hiyo.

Mwenyekiti wa Kambi ya Upinzani Mhe. Freeman Mbowe (CHADEMA) akipata maelezo kutoka kwa mtaalamu wa kampuni  ya vifaa vya umeme jua ya Ensol Tanzania Limited inayofadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Bw. Godwin Msigwa mara alipotembelea banda hilo ili kujionea shughuli zake.