Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ukipita leo katika ‘mkeka’ wa barabara, ulipokuwa ukitoka Namtumbo kwenda Songea, Kinana akiwa katika ziara mkoani Ruvuma, kukagua utelekezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kushirikiana nao kupata njia za kuzitatua, baba hiyo ni miongozi mwa barabara kadhaa zilizojengwa katika maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya CCM na kuwaondolea wananchi kero ya kusafiri kwenye barabara mbovu.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa nyumba ya mwalimu kwenye shule ya sekondari Mdandamo wilayani Songea mjini
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikagua ujenzi wa nyumnba ya maabara katika shule hiyo
Katibu wa NEC, Itikati na Uenezi Nape Nnauye akishirikiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wai Ruvuma, kuondosha gogo kwenye eneo la ujenzi wa Zahanati katika Kata ya Mahilo, Songea mkoani Ruvuma
Wazee pekee wawili walisosalia kati ya waliokuwepo kwenye mkutano wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere wakati wa harakati za TANU, mwaka 1957 katika eneo la Matogolo, Songea mkoani Ruvuma, Hashim Gawaza (92) na Clemence Simon Nyoni (93), wakivishwa vazi la heshima na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alipowasili eneo hilo leo
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akiwa na Wazee hao
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (kushoto) akiwa na wanachama wa Shina namba noja, waliokuwa wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alipotembelea nyumbani kwa Mjumbe wa Shina namba moja, Magreth Mtiula, eneo la Mfaranyaki mjini Songea.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na muasisi wa TANU na baadaye CCM, Mzee Mustafa Songambele, baada ya kuzungumza na wanachama kwenye shina namba moja mjini Songea
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akisalimiana na Mzee Songambele mjini Songea
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimsalimia mama huyu, Mkazi wa mtaa wa Mfaranyaki mjini Songea, baada ya kumuona kuwa mwenye shangwe kubwa wakati msafara wa Kinana ulipopita karibu na nyumbani kwa mkazi huyo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akifungua Shina la Vijana Wajasiriamali wa CCM la Dk. Asha-Rose Migiro, katika mtaa wa Mfaranyaki mjini Songea leo
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akisalimia baada ya kuzinduliwa shina hilo. Imetayarishwa na theNkoromo Blog