BARAZA la Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limewataja waamuzi tisa na waamuzi wasaidizi tisa watakao chezesha Mashindano ya Kombe la CECAFA Chalenji. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Ofisa Habari wa CECAFA, Rogers Mulindwa waamuzi hao wanatoka katika nchi 12 ambazo ni wanachama wa baraza hilo.
Marefarii waliotajwa ni pamoja na Anthony Okwayo- Kenya, Denis Batte- Uganda, Wish Yabarow- Somalia, Israel Mujuni- Tanzania, Louis Hakizimana- Rwanda, ThieryNkurunziza- Burundi, WaziriSheha- Zanzibar, GebremichaelLuleseged- Eritrea pamoja na KheiralaMurtaz kutoka Sudan.
Waamuzi wasaidizi ambao wametajwa pia, yumo Gilbert Cheruiyot- Kenya, TonnyKidiya- Kenya, Mark sonko- Uganda, FedinardChacha- Tanzania, Suleiman Bashir- Somalia, Fraser Zakara-South Sudan, SimbaHonore- Rwanda, Hamid Idam- Sudan na KinfeYimla- Ethiopia/
Mashindano ya CECAFA Chalenji mwaka huu yanatarajia kuanza Novemba 27 na kuzishirikisha nchi wanachama za Burundi, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Sudan, Somalia, South Sudan, Tanzania, Uganda pamoja na Zanzibar (Tanzania).