Meneja Mauzo ya rejareja wa Samsung Tanzania Bw. Sylvester Manyara akionyesha bidhaa mbalimbali za Samsung zitakazoshindaniwa kwenye shindano la Pambika na Samsung katika uzinduzi wa promosheni hiyo iliyofanyika leo katika duka la Samsung Quality Center, Dar es Salaam.
Meneja Mkuu wa Samsung Tanzania, Bw. Kishor Kumar akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi rasmi wa promosheni kabambe ya Pambika na Samsung inayolenga kuwazawadia wateja watakaonunua bidhaa za Samsung na kuzisajili zawadi mbalimbali kila. Tukio hilo limefanyika katika Duka la Samsung liliopo Quality Center, Dar es Salaam.
Bw. Kishor Kumar, Meneja Mkuu wa Samsung Tanzania (kushoto) akionyesha zawadi kubwa ya gari aina ya Mitsubishi Pick-up mpya mbele ya wanahabari (hawapo pichani) kulia ni Sylvester Manyara Meneja Mauzo Rejareja wa Samsung Tanzania. Mteja mmoja wa Samsung atajiondokea nyumbani na gari hilo litakalosheheni bidhaa mbalimbali kutoka Samsung katika droo ya mwisho ya Novemba 23, 2013 itakayofanyika katika eneo la Kibiashara la Mlimani City, Dar es Salaam.
KAMPUNI inayoongoza kwa uuzaji wa vifaa vya kielektroniki nchini Tanzania, imetangaza kuanza rasmi kwa kampeni yake kabambe itayoyotoa zawadi kwa wateja wake wakati wa msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka. Hii itakuwa ni moja kati ya promosheni kubwa kufanywa na Samsung nchini Tanzania. Promosheni hiyo itakayodumu kwa muda wa wiki sita itawapa wateja wenye bahati nafasi ya kushinda bidhaa za Samsung na mteja mmoja wa Samsung atazawadiwa gari jipya aina ya Mitsubishi Double Cabin ikiwa imejaa bidhaa zote kutoka Samsung katika droo ya mwisho.
Akizungumza na waandishi wa Habari katika uzinduzi wa promosheni ya Pambika na Samsung, Meneja Mkuu wa Samsung Tanzania Bw. Kishor Kumar alisema “Msimu wa sikukuu upo karibu, tunatambua kwamba wateja wetu wanatumia msimu huu kufurahi na kuonyesha upendo kwa kupeana zawadi na familia pamoja na marafiki”
“Samsung hatutengenezi tu bidhaa bora ila pia tunatengeneza Jukwaa la kutoa fursa kwa watu wetu kufurahia maisha yao kwa kupitia bidhaa zetu na teknolojia zetu ili kuwawezesha kuonyesha vipaji vyao kwa kadri wanavyoweza. Kuongeza wigo wa kufaidika na bidhaa za Samsung kwa wateja wetu, hii itawapa nafasi Watanzania wote kuwa na ndoto za kumiliki bidhaa bora za Samsung kwa kusajili tu IMEI namba za simu zao mara wanaponunua, promosheni hii tumeipa jina la Pambika na Samsung” alisema Bw. Kishor
Akisoma hotuba yake mbele ya waandishi wa habari wakati wa Uzinduzi wa Pambika na Samsung, Bw. Kishor Kumar aliongeza “Kuanzia leo, tutakuwa tukishuhudia Zawadi bora kutoka Samsung kama; kompyuta mpakato, jiko la umeme, luninga ya inchi 32 yenye teknolojia ya LED, Muziki wa nyumbani, Kompyuta ya mkononi aina ya Galaxy, mashine ya kufulia nguo, jokofu na deki za DVD, zote zinawasubiria wateja watakaonunua bidhaa za Samsung kushinda kila wiki katika kipindi cha wiki 6 mfululizo. Mshindi wa zawadi kubwa mwenye bahati atachaguliwa Desemba 23, 2013 ambapo ataondoka nyumbani na gari mpya aina ya Mitsubishi Pick-up iliyosheheni zawadi kibao toka Samsung”
Pambika na Samsung ni promosheni ya nchi nzima kuanzia Novemba 7 mpaka Desemba 23, 2013. Promosheni hii ina lengo la kuwazawadia wateja wa Samsung wakati huo huo ikihamasisha wateja wake kujisajili katika huduma muhimu ya E-Warranty ili mteja aweze kufurahia faida lukuki za kutumia bidhaa halisi za Samsung.
Kushiriki katika Pambika na Samsung ni rahisi sana, unachotakiwa ni kununua bidhaa mpya ya Samsung na kutuma ujumbe mfupi wenye na namba ya utambulisho wa simu yako yani namba za IMEI kwenda 15685. IMEI namba ni namba maalum kumi na tano zinazothibitisha umilikaji wa simu yako, namba hizo zipo nyuma ya boksi la simu uliyonunua, au chini ya betri yako, au piga *#06#.
Samsung kila siku inatengeneza fursa na Pambika na Samsung ni moja kati ya fursa ambayo inamuwezesha mteja kumiliki simu yake. Promosheni hii ina lengo la kuwazawadia wateja wa Samsung wakati huo huo ikihamasisha wateja kujisajili na huduma ya miezi 24 ya E-Warranty ili kuweza kufurahia faida za kutumia simu na bidhaa halisi za Samsung.