Na Magreth Kinabo – MAELEZO
NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel amewataka wasanii nchini kutumia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kwa ajili ya kukopa fedha za kuendeleza kazi zao.
Profesa Gabriel alisema hayo jana wakati alipokutana na baadhi viongozi wa mashikisho ya wasanii na wasanii kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa wizara hiyo.
Alisema Serikali imetenga fedha kiasi cha Sh. bilioni 6.1 kupitia mfuko huo, ambapo kati ya fedha hizo Sh. bilioni 1.4 za makundi maalum wakiwemo wasanii. Hivyo ni vyema wasanii vijana wakaanza kutumia fursa hiyo. Wakati huohuo Naibu Katibu Mkuu huyo aliwataka wasanii kuzingatia maadili na kujenga heshima katika utendaji wa kazi zao michango ya iendelea kutambulika kwenye jamii.
Profesa Gabriel aliyasema hayo jana wakati alipokuwa akifunga warsha ya siku moja kuhusu Haki miliki kwa wasanii iliyofanyika kwenye ukumbi wa Nyumbani Lounge, Namanga jijini Dar es Salaam.
Alitoa wito kwa wasanii hao kuacha kusema kwani tabia hiyo inaharibu majina yao kwa kuwa itakuwa ni vigumu jamii kuthamini michango yao iwapo watajihusisha na vitendo viovu, huku akisisitza kwamba wasanii ambao majina yao yameshajengeka katika jamii watambue kuwa huo ni mtaji wao wasiupoteze.
Aliwataka kuanza kufanya kazi zao kibiashara na kuwa taaluma ya biashara ili waweze kuifanya kazi hiyo kwa ufanisi, ikiwemo kutumia mapato ya kazi zao katika kufanya shughuli zingine. Alisema Serikali itaendelea kushirikiana na wasanii katika kukabiliana na changamoto mbalimbali wanazozikabili.
Kwa upande wake msanii maarufu John Kitime akizungumza kwa niaba ya wenzake alivitaka vyombo vya habari viwe vinalipia kazi zao wasanii pale wanapotumia nyimbo zao.
Naye mmoja wa kiongozi, Rais Shirikisho la Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifamba aliomba wapewe nguvu ya kisheria ili kuweza kudhibiti maadili ya wasanii kauli ambayo ilingwa mkono na baadhi ya viongozi wenzake.
Kwa upande wao wasanii hao, waliiomba Serikali kutawasaidia kutatua tatizo la uharamia wa kazi za wasanii, ambapo Suzan Lewis alishauri kuwa ikiwezekana utumika mfuko unatumika kwenye vocha za simu ambazo mtu hawezi kughushi. Pia walipendekeza kuwepo kwa bei elekezi ili kudhibiti uuzaji holela kwa kazi zao.