Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), mkoani Mbeya kinatarajia kufanya maandamano
makubwa, kesho Jumapili Julai 16, yatayofuatiwa na mkutano wa hadhara
utakaofanyika katika viwanja vya Luanda Nzovwe, jijini Mbeya.
Maandamano hayo yatakayoanzia eneo la Mafiati na kuishia viwanja vya
Luanda Nzovwe, yatawashirikisha wana-CCM, wapenzi na wananchi wa jiji
la Mbeya na vitongoji vyake.
Maandamano hayo yatapokewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC)
ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, ambaye ataongozana na Katibu
wa NEC ya CCM, Oganaizesheni, Asha Abdalah Juma.
Viongozi wengine watakaokuwepo na watakaohutubia mkutano huo ni pamoja
na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, ambaye pia ni
Waziri wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta, Naibu Waziri wa Ujenzi Dokta
Harrison Mwakyembe, Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko na
mbunge wa jimbo la Singida , Razaro Nyarandu mbunge wa Same
mashariki, Anne Kilango Malecela na mbunge wa Simanjiro, Christopher
Ole Sendeka.
Lengo la maandamano na mkutano huu ni kuelezea maendeleo ya zoezi la
mageuzi ndani ya CCM kwa lengo la kujiimarisha, na kujibu hoja
zilizotolewa na wapinzani katika mikutano yao waliyoifanya hivi
karibuni katika jiji la Mbeya na maeneo mengine nchini.
Imetolewa na
Bashir Madodi
Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM mkoa wa Mbeya,