Julias Nyaisanga Aagwa Dar, Mbowe Atoa Changamoto kwa Wanahabari

 

IMG_0052

 

Mmoja wa Maofisa wa ngazi za Juu wa Jeshi la Polisi kutoka Kitengo cha Upelelezi Makao Makuu, Jamal Rwambow akitoa heshima za mwisho mbele ya mwili wa Julias Nyaisanga katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.

IMG_0054

Baadhi ya waandishi wa habari wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Nyaisanga katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.

IMG_0038

 

Anko Kitime (mwenye fulana nyeupe) akipita kutoa heshima za mwisho kwenye jeneza la mwili wa marehemu Nyaisanga viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.

IMG_0098

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akizungumza na wanahabari kwenye Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.


IMG_0078

Mjane wa marehemu akiwa na ndugu wa karibu wa marehemu Nyaisanga viwanja vya Leaders.

IMG_0067

Baadhi ya waombolezaji wakitia saini kitabu cha maombolezo cha Julias Nyaisanga viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.

IMG_0056 IMG_0033

Waombolezaji wakitoa salamu za mwisho kwenye jeneza la marehemu Nyaisanga.

IMG_0008

IMG_0104

 

Jeneza la mwili wa marehemu Julias Nyaisanga ukiingizwa kwenye gari tayari kwa kusafirishwa kuelekea Tarime kwa mazishi.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika Kitabu cha maombolezo ya Kifo cha aliyewahi kuwa mtangazaji wa Redio Tanzania, ITV na Redio One na Redio Aboud, marehemu Julius Nyaisanga, aliyefariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita huko mjini Morogoro kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu. Marehemu Nyaisanya ameagwa leo katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni na anasafirishwa leo hii kuelekea Tarime kwa ajili ya maziko. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa aliyewahi kuwa mtangazaji wa Redio Tanzania, ITV na Redio One na Redio Aboud, marehemu Julius Nyaisanga, aliyefariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita huko mjini Morogoro kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu. Marehemu Nyaisanya ameagwa leo katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni na anasafirishwa leo hii kuelekea Tarime kwa ajili ya maziko.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji mfiwa Leah Nyaisanga, ambaye ni mke wa marehemu wa aliyewahi kuwa mtangazaji wa Redio Tanzania, ITV na Redio One na Redio Aboud, marehemu Julius Nyaisanga, aliyefariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita huko mjini Morogoro kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu. Marehemu Nyaisanya ameagwa leo katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni na anasafirishwa leo hii kuelekea Tarime kwa ajili ya maziko.
 Leah Nyaisanga, ambaye ni mke wa marehemu wa aliyewahi kuwa mtangazaji wa Redio Tanzania, ITV na Redio One na Redio Aboud, marehemu Julius Nyaisanga, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu mumewe, aliyefariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita huko mjini Morogoro kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu, wakati wa shughuli za kuagwa mwili huo zilizofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club Kinondoni na anasafirishwa leo hii kuelekea Tarime kwa ajili ya maziko.
 Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda (kulia) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, wakati wa shughuli hiyo Viwanja vya Leaders.
 Sehemu ya Wanakamati wa Kamati ya maziko…!
 Sehemu ya waombolezaji waliojitokeza kumuaga marehemu Nyaisanga, katika Viwanja vya Leaders Club.
 
 Sehemu ya waombolezaji waliojitokeza kumuaga marehemu Nyaisanga, katika Viwanja vya Leaders Club.
 

Na Joachim Mushi

MAKAMU Rais wa Tanzania, Dk. Mohamed Gharib Bilal leo amewaongoza mamia ya waombolezaji, baadhi ya viongozi, wadau wa masuala ya habari, na wanatasnia nzima ya habari kutoa salamu za mwisho kwa aliyekuwa mtangazaji maarufu nchini marehemu Julias Nyaisanga.

Shughuli hizo zimefanyika kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam kuanzia majira ya asubuhi, huku makundi anuai yakipata fursa ya kutoa hotuba wakimzungumzia marehemu Nyaisanga aliyefaamika zaidi kwa jina la utani Anko J wakati wa uhai wake.

Katika hotuba za makundi kadhaa yaliopata fursa ya kumzungumzia marehemu Julias Nyaisanga, mengi yameonekana kumsifu kwa uhodari wake katika kazi enzi za uhai wake pamoja na ushirikiano aliokuwa nao kwenye tasnia nzima ya habari.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akizungumza na wanahabari kwenye viwanja hivyo, aliwataka wanahabari kwenda mbele zaidi kwa kuanza kuandika historia za waandishi wa habari kuelezea mchango wao katika jamii na masuala mbalimbali ya kukumbukwa wanayoyafanya ili kubaki na historia kwa vizazi vijavyo.

Alisema kila mtu ana historia ya kufaa kuwekwa kwenye kumbukumbu haswa vitabu hivyo tamaduni za kuanza kuandika historia kwa watu kama akina Julias Nyaisanga itasaidia sana kujifunza kwa vizazi vya baadaye.

“Tujifunze namna ya kuweka kumbukumbu za taifa kwa kuandika historia za watu mbalimbali…waandishi wa habari jengeni utamaduni wa kuandika historia sio zenu tu na hata za watu wengine mfanye utafiti itasaidia kuweka kumbukumbu na mtapata rejea muhimu sana katika maisha ya baadaye.”

“Nyaisanga amefanya mambo mengi katika nchi hii kuna kipindi alikuwa DJ mkubwa sana na maarufu kwa miaka fulani lakini leo ameondoka vijana wengi wadogo hawata weza kujua historia ya mtu huyu, sasa ni vema kama taifa na hasa waandishi wa habari hebu anzeni utamaduni wa kuandika historia za watu pia za viongozi na watu wengine maarufu…,” alisema Mbowe.

Naye Msemaji wa Serikali ya Tanzania na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Assah Mwambene akimzungumzia marehemu, alisema kifo chake kimeacha pengo kubwa kwa tasnia ya habari na familia yake kutokana na mchango aliyokuwa nao.

Mwambene alisema Nyaisanga alikuwa maarufu kutokana na kufuata weledi na maadili ya tasnia na pia ni miongoni mwa walimu wazuri waliokuwa wakiwanoa wanahabari tangu akiwa Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD). “…Kwa kweli ameacha pengo kubwa kwa familia pamoja na taifa kwa ujumla…mazuri ambayo tunaweza kumkumbuka Nyaisanga ni weledi na kufuata maadili ya kazi alipokuwa anatangaza ni mara chache sana utamkuta akibabaika ama kutamka maneno visivyo (kukosea), lakini pia alikuwa mwalimu mzuri kwa watu ambao tulipata nafasi ya kufanya naye kazi…,” alisema Mwambene.

Marehemu Nyaisanga ambaye alifariki Oktoba 20, 2013 mjini Morogoro alizaliwa Januari Mosi mwaka 1960 na amewahi kufanya kazi katika vituo anuai vya radio ikiwa ni pamoja na RTD, Radio One na kwa sasa hadi mauti yanamkuta alikuwa Mkurugenzi wa Abood Media ya mkoani Morogoro.

Marehemu Nyaisanga amesafirishwa leo kwa gari kuelekea Tarime kwa mazishi. Mtandao wa dev.kisakuzi.com unatoa pole kwa wanatasnia familia na taifa kwa ujumla kwa kifo cha Nyaisanga. Bwana ametwaa na jina lake lihimidiwe, amina.