Makamu wa Rais Tanzania Afungua Mkutano wa Vyombo vya Habari na Utangazaji

IMG_8277
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mkurugenzi mkuu wa TCRA Profesa John Mkoma nje ya ukumbi wa mikutano wa A I C C jijini Arusha, baada ya kufungua  mkutano mkuu wa 21 wa Vyombo vya Habari na Utangazaji kwa nchi za Kusini mwa Afrika (SABA) leo 21 Oktoba 2013.

IMG_8268
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, katikati akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano mkuu wa 21 wa Vyombo vya Habari na Utangazaji kwa nchi za Kusini mwa Afrika (SABA) baada ya kufungua mkutano huo leo 21 Oktoba 2013 katika ukumbi wa A I C C Arusha.

IMG_8240
Baadhi ya washiriki wa mkutano mkuu wa 21 wa Vyombo vya Habari na Utangazaji kwa nchi za Kusini mwa Afrika (SABA) wakimsikiliza Makamu wa Rais Dk Mohammed Gharib Bilal, alipokua akifungua mkutano huo leo Oktoba 21 2013 katika ukumbi wa A I C C jijini Arusha.

IMG_8287
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na wasanii wa ngoma ya kimasai waliokua wakitumbiza nje ya ukumbi wa mikutano wa A I C C jijini Arusha, baada ya kufungua mkutano mkuu wa 21 wa Vyombo vya Habari na Utangazaji kwa nchi za Kusini mwa Afrika (SABA) leo 21 Oktoba 2013. (Picha na OMR)