Matukio Ziara ya Rais Kikwete Njombe

l2

l5

 

Rais Jayaka Mrisho Kikwete akikagua  sehemu mbalimbali za kiwanda cha chai cha Ikanga wilaya ya Njombe baada ya kukifungua leo Oktoba 18, 2013

l9

 

Rais Jayaka Mrisho Kikwete akikagua  sehemu mbalimbali za kiwanda cha chai cha Ikanga wilaya ya Njombe baada ya kukifungua leo Oktoba 18, 2013

l12

 

l10

 

Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakikagua chai ikichambuliwa katika kiwanda cha chai  cha Ikanga, Njombe,  ikiwa ni sehemu ya  sherehe za uzinduzi rasmi wa mkoa mpya wa Njombe Ijumaa Oktoba 18, 2013.

l1

 

Rais Jakaya Kikwete akiambatana na Mkewe Mama Salma Kikwete wakipokea taarifa fupi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mufindi Tea Company Group Bwana Noel Smith, kuhusu kukamilika kwa kiwanda cha chai walichokijenga katika kijiji cha Ikanga kilichoko katika Kata ya Lupembe, wilayani Njombe ambacho Rais Kikwete alikizindua  rasmi tarehe 18.10.2013.

IMG_4424

 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibofya kitufe huku  wazee wa Njombe wakirusha njiwa kuashiria kuzinduliwa rasmi mkoa wa Njombe leo Oktoba 18, 2013 katika Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe.

IMG_4340

IMG_4336

 

Chipukizi wa Mkoa wa Njombe wakicheza halaiki wakati wa sherehe ya ufinguzi rasmi wa Mkoa wa Njombe zilizofanyika tarehe 18.10.2013.

IMG_4219

 

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiangalia bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na akinamama wa kikundi cha Jitegemee wakati wa maonyesho yaliyofanyika mjono Njombe kwa ajili ya sherehe za uzinduzi rasmi wa mkoa wa Njombe huku kiongozi wa kikundi hicho Mama Leokadia  Kaduma akimfafanulia juu ya bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na wanakikundi hao.

IMG_4054

 

Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiangalia chai iliyosindikwa na kufikia hatua ya mwisho kabla ya kufungwa kwenye pakiti huku wakipata maelezo kutoka kwa Meneja Msaidizi wa Kiwanda cha chai cha Ikanga  Bwana Flowin Msigwa .

IMG_3989

 

Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiangalia majani ya chai yaliyofikishwa katika kiwanda cha chai cha Ikanga kwa ajili ya kusindikwa. Kiwanda hicho kilizinduliwa rasmi na Rais Kikwete tarehe 18.10.2013. (PICHA NA JOHN LUKUWI NA IKULU)