Silima Kufungua Kikao cha Bajeti ya Magereza

Kikao hicho kitarajiwa kufungwa Oktoba 22  mwaka huu na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Bw.John Minja.

Kikao hicho kitarajiwa kufungwa Oktoba 22 mwaka huu na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Bw.John Minja.

Na Lorietha Laurence-Maelezo

NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Pereira Silima atafungua kikao cha bajeti ya Magereza kwa mwaka wa fedha2013/2014 Oktoba 21 mwaka huu mjini Morogoro.

Kikao hicho kitashirikisha wajumbe 94 wakiwemo maafisa waandamizi kutoka makao makuu ya Jeshi la Magereza,Wakuu wa Miradi ya Magereza na wasimamizi wa miradi hiyo.

Katika kikao hicho wajumbe watajadili taarifa za utekelezaji wa bajeti iliyopita ya mwaka wa fedha 2012/2013 kwa kuangalia mafanikio na changamoto zilizojitokeza kwa kipindi hicho na kuwasilisha bajeti ya mwaka wa fedha 2013/2014.

Shirika la Magereza linashughulika na miradi mbalimbali ya kiuchumi ambayo ni kilimo , mifugo , viwanda vya kutengeneza viatu,sabuni,samani za ofisini na majumbani pamoja na uzalishaji wa chumvi.

Kikao hicho kitarajiwa kufungwa Oktoba 22 mwaka huu na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Bw.John Minja.