Mwili wa Mama Ufoo Saro Wasafirishwa, Mashuhuda Wazungumzia Mauaji…!

Goodlack mtoto wa Ufoo Saro akiuaga mwili wa bibi yake kanisaniMtoto wa Ufoo Saro akiuaga mwili wa bibi yake aliyeuwawa kwa risasi na baba yake kanisani Kibamba”

Wengine walishindwa kujiweza na kusaidia baada ya majonzi ya kuona maiti.1Wengine walishindwa kujiweza na kusaidia baada ya majonzi ya kuona maiti.

Baadhi ya ndugu wa karibu wa Anastazia Saro  wakiwa kanisani kwenye ibada. Baadhi ya ndugu wa karibu wa Anastazia Saro wakiwa kanisani kwenye ibada.

Gari lililobeba mwili wa Marehemu Anastazia Soro likiwa Muhimbili  kabla ya kuanza safari. Gari lililobeba mwili wa Marehemu Anastazia Soro likiwa Muhimbili kabla ya kuanza safari.

Hapa napo nao wanajaribu kuwapiga picha wanahabari ambao walikuja kushuhudia tukio hilo. Hapa napo nao wanajaribu kuwapiga picha wanahabari ambao walikuja kushuhudia tukio hilo.”

Hii ndio nyumba ambapo yalifanyika mauaji. Ndio nyumbani kwa akina Ufoo Saro. Hii ndio nyumba ambapo yalifanyika mauaji (yenye bati la kijani). Ndio nyumbani kwa akina Ufoo Saro.”

Jeneza likiingizwa kwenye gari tayari kwa safari kuelekea Moshi “Jeneza likiingizwa kwenye gari tayari kwa safari kuelekea Moshi”

Jeneza likiingizwa kwenye gari tayari kwa safari kuelekea Moshi.1Jeneza likiingizwa kwenye gari tayari kwa safari kuelekea Moshi.

Kwa heri Bibi...! ndivyo anavyoelekea kusema mtoto wa Anthery Mushi, Goodlack anayeaga mwili wa bibi yake kanisani.“Kwa heri Bibi…!”.. ndivyo anavyoelekea kusema mtoto wa Anthery Mushi, anayeaga mwili wa bibi yake kanisani.

Muhimbili nje ya chumba cha kuhifadhia maiti.Muhimbili nje ya chumba cha kuhifadhia maiti.

Mwili wa Anastazia Saro ukiingizwa kwenye gari tayari kuelekea Kimbamba nyumbani kwa marehemu.Mwili wa Anastazia Saro ukiingizwa kwenye gari tayari kuelekea Kibamba nyumbani kwa marehemu.

Na Mwandishi Wetu

MAMA wa mtangazaji wa ITV, Ufoo Saro aliyeuwawa kwa risasi juzi nyumbani kwake, Kibamba CCM, eneo la Kibwegere, Anastazia Saro ameagwa leo na kusafirishwa kuelekea Machame, Kijiji cha Shari Wilaya ya Hai, Mkoani Kilimanjaro kwa mazishi.

Mwili wa Anastazia saro mama mzazi wa Ufoo Saro ulitolewa Chumba cha kuhifadhia maiti Muhimbili majira ya saa sita kasoro na kupelekwa eneo la Kibwegere nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, ambapo ibada ya kumuombea marehemu ilifanywa katika Kanisa la KKKT, Usharika wa Pwani, Jimbo la Magharibi Mtaa wa Kibwegere.

Majonzi, simanzi, hudhuni na vilio ndivyo vilivyotawala nyumbani kwa marehemu baada ya mwili kuwasili eneo hilo na baadaye hali hiyo pia kuhamia kanisani wakati wa kuaga mwili wa marehemu Anastazia kabla ya kuanza msafara wa kuelekea Machame kwa mazishi.

Mwandishi wa dev.kisakuzi.com aliyekuwa akifuatilia matukio yote tangu Muhimbili alishuhudia baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wakishindwa kujizuia na kuangua kilio huku baadhi ya ndugu kupoteza fahamu kwa kuzidiwa na majonzi. Akisoma salamu za shukrani mmoja wa wasemaji wa familia alisema madaktari baada ya uchunguzi wa mwili wa marehemu ametoa jumla ya risasi tano ambazo ndizo zinadaiwa kusababisha kifo cha mama huyo.

Marehemu Anastazia ambaye pia alikuwa mwimbaji kwaya katika kanisa hilo, ilipofanyika ibada ya kumuombea kabla ya kusafirisha wanakwaya walionekana kushindwa kujizuia na kulia kwa uchungu hasa walipokuwa wakitoa salamu za mwisho. Marehemu alizaliwa mwaka 1957.

Wakielezea walichoshuhudia kabla ya kutokea kwa mauaji hayo baadhi ya majirani wa Anastazia Saro walisema, Anthery Mushi ambaye ni mzazi mwenzie Ufoo Saro alifika kwa akina Saro siku moja kabla ya mauaji na kufanya mazungumzo na marehemu kisha aliondoka lakini kilometa chache aliegesha gari lake na kukaa eneo hilo hadi saa saba usiku.

“Mimi nafanya kazi baa moja ambayo si mbali sana na nyumba ya marehemu, siku moja kabla ya mauaji Mushi alifika jioni na kufanya mazungumzo na marehemu lakini haikujulikana walichozungumza…baada ya kumaliza mazungumza aliondoka nyumbani kwa akina Ufoo na kwenda kuegesha gari barabarani kilomita chache kutoka pale, eneo hilo alikaa hadi usiku,” alisema mmoja wa mashuhuda akizungumza na mtandao huu.

“Mimi niliondoka pale baa majira ya saa saba usiku alikuwa bado kaegesha gari pale pale huku akiwa ndani ya gari haikujulikana alikuwa anafanya nini…baadhi wanahisi alilala pale pale,”

“Inasemekana asubuhi alirudi nyumbani kwa akina Ufoo akiwa mwenyewe na baadaye aliwasili Ufoo na gari lingine na wote kuingia ndani kwa mazungumzo…muda mfupi ndipo ikaanza kusikika milio ya risani zikipigwa ndani ya nyumba hiyo,” alisema shuhuda huyo.

Alisema kwa mujibu wa taarifa walizozipata kwa baadhi ya ndugu wa familia ya akina Ufoo, Mushi alitaka kuwauwa wote waliokuwa ndani ya numba hiyo na kuiteketeza kwa moto lakini majirani waliwahi kuuzima moto huo ambao aliuwasha jikoni baada ya kupiga risasi mtungi wa gesi.

Ndugu wa Ufoo walilazimika kujifungia katika moja ya chumba ambacho Mushi alijitahidi kuvunja kitasa kwa kutumia risasi ili kufungua mlango wa chumba hicho ili awadhuru lakini walimzidi nguvu kwa kuuzuia mlango usifungukea na baadaye alizunguka dirishani na kupiga risasi kuelekea chumba hicho lakini tayari walikuwa wamejificha kwa kupanda darini ndani ya chumba hicho.

Taarifa ambazo zimepatikana kutoka kwa majirani wa Mushi waliozungumza na dev.kisakuzi.com kutoka Uru-Timbirini, Mkoani Kilimanjaro, ambazo hata hivyo hazikuweza kuthibitishwa zinasema ugomvi uliokuwepo kisha ni nyumba. Inasemekana Mushi alituma fedha akiwa Darfur wakikibaliana na mzazi mwenzake ijengwe nyumba nyumbani kwao Uru-Timbirini lakini haikujengwa na baada ya yeye kurudi ghafla na kufika nyumbani kwao na kukuta hakuna kitu nipo alipokuja Dar es Salaam kufanya mazungumzo na Ufoo pamoja na familia yao.

Hata hivyo bado kuna usiri mkubwa juu ya ukweli wa mambo wa tukio na sababu ya mauaji hayo ya kinyama na mtu pekee ambaye atataka kuweka wazi ni Ufoo pamoja na ndugu wa Mushi.