JK Atoa Milioni 5.5 kwa Makundi Maalumu Kusheherekea Sikukuu ya Edi El Hajj

zawadi za Ed El Hajj

zawadi mbalimbali

akikabidhiwa zawadiZawadi mbalimbali zilizotolewa kwa ajili ya sikukuu ya Ed El Hajj kwa makundi maalum

NA MAGRETH KINABO – MAELEZ

RAIS Jakaya Kikwete ametoa msaada wa vyakula wenye thamani ya Sh. milioni 5.5 kwa makundi maalum ambayo ni wazee na wasiojiweza, watoto yatima na watoto walio katika mkinzano na kisheria kwa ajili ya kusherekea sikukuu ya Edi El Hajj.

Msaada huo ulitolewa leo kwa niaba ya Rais Kikwete , na Kaimu Kamishna wa Usatawi wa Jamii Rabirira Mushi katika hafla fupi iliyofanyika kwenye mahabusu ya watoto iliyopo Regency jijini Dares Salaam kwa vituo na makazi 12 ya makundi hayo yaliyopo hapa nchini.

“ Mhe. Rais ametoa zawadi ya mbuzi, mchele na mafuta ya kupikia ili kuona kwamba watoto na wazee hawa wanajumuika na wanajamii wengine katika sherehe hii,” alisema Rabirira.

Alivitaja vituo vilipokea msaada huo kuwa ni kituo cha watoto Dar Al arkam na Nunge vyote viko(Temeke), Msongola Orphaned Centre(Ilala), Furaha(Kinondoni) Mother Theresa(Mburahati), Malaika Kids Home(Mkuranga) na makazi ya wazee na wasiojiweza cha Kilima(Bukoba Vijijini).

Vituo vingine ni Mahabusi ya watoto(Arusha Mjini), mahabusi ya watoto(Tanga Mjini), makazi ya wazeee Mwanzange(Tanga), makao ya watoto Istikana (Pemba ) na makazi ya wazee Sebuleni(Unguja).

Akizungumzia kuhusu msaada huo kwa niaba ya wenzake Mwenyekiti wa kituo cha Msongola Orphaned Trust Fund, Shanta Deus alimshukuru Rais Kikwete kwa moyo wake wa kujitolea kwa makundi hayo huku akiwataka watu wengine kuiga mfano.
“Ninawaomba watu wengine, sekta binfasi na kampuni mbalimbali kuiga mfano huu ili kuweza kuwasaidia watoto yatima na wanaoshi katika mazingira hatarishi pamoja na makundi maalum kwa kutoa misaada mbalimbali,”alisisitiza Shanta.

Naye Sista Oliver Paulo ambaye ni mlezi wa makao ya watoto ya yatima, kijiji cha Furaha aliishauri jamii iwe tabia ya kushirikiana na makundi hayo katika sherehe mbalimbali na kuwasaidia.