Watoto wa Kike wa Shule ya Msingi Kisaki wakielekea shuleni, bahati mbaya viatu hakuna miguuni kutokana na hali ya umasikini kwenye familia zao. Naona hapa kuvaa viatu kwao ni hanasa.
Masomo yanaendelea…!
Hili ni darasa la tano wanafunzi wamesongamana kutokana na ukosefu wa madawati.
Shuleni nako mambo ni vile vile, madawati hakuna ya kutosha hivyo wengi hulazimika kukaa chini na kuandikia chini.
Wanafunzi wa darasa la nne wakiwa wamekaa chini wengine viatu hakuna hivyo ni peku peku ardhini. Hii ni changamoto kwa Serikali na jamii kwa ujumla.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kituoni KISAKI, Philip Kayombo akitabasamu na wanafuunzi wake katika picha. “Hali ngumu ya shule isiwe kisingizio cha kutabasam…!”
“Tumekaa chini lakini na hatuna viatu lakini mafunzo yanaendelea kama kawaida…!” Baadhi ya wanafunzi wakiwa darasani wakiendelea na vipindi.
Nyumba pekee ya walimu ambayo Mwalimu Mkuu anaitumia na walimu wengine wawili wapya ambao wameanza kazi mwaka jana. nyumba hii ina vyumba viwili na sebule. Hivyo nyumba hii wanakaa jumla ya walimu watatu.
SHULE nyingi za msingi maeneo ya vijijini zinakabiliwa na changamoto anuai katika mazingira ya elimu. Shule ya Msingi Kituoni iliyopo Kata ya Kisaki mkoani Morogoro inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo uhaba wa madawati hali inayosababisha wanafunzi kukaa chini, huku madarasa yakiwa na msongamano mkubwa kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa.
Hali ya kiuchumi kwa wazazi wengi wa shule hiyo nayo ni mbaya kiasi cha kuonekana tu kwa wanafamilia. Hii pia waweza itambua kwa kuangalia muonekano wa baadhi ya wanafunzi ambao wengi wanakuja shuleni peku yaani bila viatu huku wakiwa na sare zilizochoka kwelili. Mtandao huu ulipata fursa ya kuitembelea shule hiyo na yafuatayo ni mazingira muonekano katika picha.