Rais Kikwete Awasili Mjini Iringa, Kuhudhuria Kilele Mbio za Mwenge

i29
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Iringa mjini Mhe Msigwa katika Uwanja wa Ndege wa Nduli mjini Iringa Oktoba 13, 2013 kuhudhuria Maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenye wa Uhuru, Wiki ya Vijana na Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere zitaziofabyika Oktoba 14, 2013 katika uwanja wa Kumbukumbu ya Samora.

i25
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na kamnada wa vijana Iringa, Asas katika  Uwanja wa Ndege wa Nduli mjini Iringa Oktoba 13, 2013 kuhudhuria Maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenye wa Uhuru, Wiki ya Vijana na Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere zitaziofabyika Oktoba 14, 2013 katika uwanja wa Kumbukumbu ya Samora. PICHA NA IKULU.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete aliwasili mjini Iringa, Oktoba 13, 2013, kwa ziara ya siku mbili ya kikazi mkoani Iringa. Rais Kikwete amefuatana na Mama Salma Kikwete. Shughuli kubwa ambazo Rais atazifanya wakati wa ziara hiyo ni kushiriki Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kuwa mgeni rasmi katika Kilele cha Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka huu wa 2013 na Kilele cha Wiki ya Vijana.

Ndege iliyombeba Rais Kikwete ilitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Nduli mjini Iringa kiasi cha saa 12.20 jioni na kulakiwa na umati mkubwa wa wananchi wakiwemo wafuasi wa vyama vya siasa vikiwamo CCM na Chadema.