Gazeti Mwananchi Latoka ‘Kifungoni’

Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Limited (MCL),Tido Mhando akizungumza na waandishi wa habari jijini kuhusu kuanza uchapishaji wa gazeti la Mwananchi lililokuwa limefungiwa kwa wiki mbili. Kulia ni Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi, Dennis Msacky (Kulia kwake) na Meneja Masoko wa Kampuni hiyo, Bernard Mukasa (kushoto).

Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Limited (MCL),Tido Mhando akizungumza na waandishi wa habari jijini kuhusu kuanza uchapishaji wa gazeti la Mwananchi lililokuwa limefungiwa kwa wiki mbili. Kulia ni Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi, Dennis Msacky (Kulia kwake) na Meneja Masoko wa Kampuni hiyo, Bernard Mukasa (kushoto).

Kampuni ya Mwananchi Communications Limited, wachapishaji na wauzaji wa magazeti ya MWANANCHI, MWANASPOTI, na THE CITIZEN leo imetoa ufafanuzi katika mambo mawili, kuhusiana na tukio lililotokea hivi karibu la kufungiwa kwa gazeti lao moja.

Kwanza ni  gazeti lake  mama la MWANANCHI ambalo halikuchapishwa wala kuuzwa kwa takribani majuma mawili kwa agizo la Serikali baada ya kulifungia. Kuhusiana na hilo, wamechukua fursa na kuongelea kuhusu KUREJEA KWA UCHAPISHWAJI WA GAZETI HILO na KUUSHUKURU UMMA kwa kuwa nao bega kwa bega.

KUREJEA KWA UCHAPISHAJI WA GAZETI
Kwa mujibu wa agizo la Serikali, kutochapishwa kwa gazeti la Mwananchi kunakwisha leo, na kuanzia kesho tarehe 11.10.2013 gazeti litakuwa mitaani kama kawaida. Kwa hiyo kuanzia kesho wasomaji wa gazeti hilo maarufu wataendelea kupata gazeti lenye habari za uhakika zinazojikita kwenye umahiri, uhuru, na weledi wa uandishi na uhariri. 
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Bw Tido Mhando, magazeti hayou yataendelea kusambazwa nchi nzima na kufika mapema kabisa kote, kupitia kwa mawakala na wauzaji wake walioenea kote Tanzania.
Kwa wapenzi wa gazeti la Mwananchi waliopo jijini Dar es Salaam, kesho watauziwa magazeti na waandishi wa gazeti hilo ambao kuanzia asubuhi watakuwa mtaani wakisherehekea uhuru wao kwa kukutana na wasomaji wao moja kwa moja.
PROMOSHENI YA CHOMOKA NA MWANANCHI
Kutochapishwa kwa gazeti la MWANANCHI kwa majuma mawili kulisababisha ile promosheni ya CHOMOKA NA MWANANCHI isimame kwa muda huo huo. Tido alichukua Fursa kuwajulisha wasomaji wake kwamba promosheni hii sasa inarudi tena na inaendelea kuanzia ilipokuwa imekomea.
Zawadi za shilingi milioni moja kila siku, na zawadi za magari mapya, zitaendelea kushindaniwa na kutolewa ili kutimiza ile ahadi yetu ya kutoa zawadi zenye thamani ya jumla ya shilingi 250,000,000/=.