PSPF Yautambulisha Mpango wa Uchangiaji wa Hiari kwa Wasanii

33
Miongoni mwa mabadiliko makubwa yaliyofanywa na PSPF; 
PSPF sasa si kwa watumishi wa umma pekee bali hata wanamuziki, waigizaji, wachezaji na hata watu wengine waliokwenye sekta zisizo rasmi wanaweza kujiunga na kufaidika na mafao yanayotolewa na mfuko huo.
 
 
Elizabeth Michael (Lulu) na Flaviana Matata.
Steve Nyerere
Meneja wa Mawasiliano, Masoko na Uenezi wa PSPF, Costantina Martin
 
Meneja wa Mawasiliano, Masoko na Uenezi wa PSPF, Costantina
Martin anasema lengo la kukukutana na wadau hawa ni kutambulisha kwao mpango wa
uchangiaji wa hiari (PSPF SUPPLIMENTARY SCHEME-PSS) ambao unamwezesha mtu
yeyote kujiunga na mpango huo awe ameajiriwa au amejiajiri mwenyewe.
 
“Uzuri wa mpango huu wa uchangiaji wa hiari, unaruhusu hata
wanachama waliokwenye mifuko mingine kujiunga nao lakini pia mwanachama
anayohiari ya kuhamia kwenye mpango wa uchangiaji kwa mujibu wa sheria yaani
Main Scheme” Anasema Costantina
 
Anasema kuwa kiasi cha michango kwenye mpango wa hiari
kinaanzia shilingi elfu kumi (10,000) kwa mwezi na hakuna kiwango cha juu
ambapo mwanachama yuko huru kuchagua kuwasilisha michango kwa wiki, mwezi au
kwa msimu na michango hiyo inawasilishwa kupitia akaunti ya benki, au wakala wa
malipo wa M-Pesa na Airtel Money.
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu
 
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu anasema mpango wa
hiari ni mkombozi kwa wadau wa sanaa na michezo kwa kuwa utawawezesha kujiwekea
akiba itakayowasaidia wakati na hata baada ya kustaafu kufanya shughuli zao.
 
Katika kuhakikisha kuwa elimu ya uhifadhi inawafikia watu
wengi na kuwahamasisha kujiunga na mpango huo waa hiari PSPF imekusudia
kuwafanya wasanii na wanamichezo kuwa mabalozi katika kufikisha elimu hiyo kwa
jamii.
 
“Sio jambo rahisi kuielimisha jamii juu ya kujiwekea akiba
kwa ajili ya maisha yao ya baadaye lakini kupitia wasanii na wanamichezo
tunaweza kuleta mabadiliko na kufanya watu wengi kuwekeza katika mifuko ya
hifadhi ya jamii” anasema Mayingu
 
Shuhudia picha za tukio zima la hafla ya chakula cha mchana kwa wadau wa sanaa na michezo iliyoandaliwa na PSPF.
 
Wadau wa sanaa.
 Afisa Mahusioano wa PSPF, Fatma Elhagy akiwa na mtumishi mwenzake.
Ofisa Mawasiliano na Masoko wa PSPFHawa Kikeke.
 Naibu Mkurugenzi wa Michezo, Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo Juliana Yasoda.
Mdau wa sanaa na akiwa na staa wa kesho.
Wadau wa sanaa na michezo.
 Baadhi ya watumishi wa PSPF.
 Mshereheshaji katika hafla hiyo, Angela Bondo.
 Baadhi ya mameneja na wakurugenzi wa idara mbalimbali wa PSPF
Wadau 
 Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa miguu kwa wanawake, Amina Karuma akiwa na Nahodha wa timu ya Taifa ya soka kwa wanawake Sophia Mwasikili.
 Elizabeth Michael (Lulu) na Flaviana Matata.
 Mr. Tairo kutoka Bodi ya Filamu Tanzania.
 Mdau
Kocha msaidizi wa klabu ya Simba Jamuhuri Kiwelu Julio nae alikuwepo.
 Columba Samjela kutoka Umoja wa Washereheshaji.
 Meneja Matekelezo wa PSPF, Amin Labani.
Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji PSPF, Frances Mselemu.
 Mwendo ni ‘kujisevia’
  
 Wadau wa sanaa na michezo 
 Baadhi ya watumishi wa PSPF katika picha ya pamoja. Wadau wengi wa tasnia ya sanaa na michezo walijitokeza kwenye halfa hiyo tukianza na Elizabeth Michael Lulu, Mwanamitindo mwenye mafanikio makubwa ndani na nje ya nchi, Flaviana Matata, Mtitu, Steve Nyerere, Nahodha wa timu ya taifa ya soka wanawake Sophia Mwasikili na wadau wengine wengii…