Mkutano wa Jukwaa la Katibu Mkuu wa EAC Waanza Nairobi

Katibu Mkuu wa EAC, Dk. Richard Sezibera

Katibu Mkuu wa EAC, Dk. Richard Sezibera


 
Na Issac Mwangi, EANA, Arusha

MKUTANO wa pili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wa Jukwaa la Katibu Mkuu wa EAC na Sekta binafsi, asasi za kiraia na wadau wengine unafanyika jijini Nairobi, Kenya kwa siku mbili kuanzia Oktoba 7, 2013.

“Jukwaa la Katibu Mkuu wa EAC linalenga kutoa nafasi ya majadiliano kati ya Katibu Mkuu wa EAC, sekta binafsi, asasi za kiraia na wadau wengine juu ya namna ya kuboresha mtangamano wa EAC kwa kuongeza kasi ya maendeleo katika kanda,” alisema Naibu Katibu Mkuu wa EAC anayeshughulikia Tija na Sekta za Jamii, Jesca Eriyo.

“Mkutano huo unatarajiwa kuja na maazimia ya wazi yanaweweza kutekelezeka kwa Katibu Mkuu ili kuweza kuyafikiria,” aliongeza.

Jukwaa hilo pia lina lengo la kuongeza ushiriki wa sekta binafsi, asasi za kiraia na wadau wengine katika uandaaji wa sera na maamuzi. Kutokana na majadilaiano kama hayo, inatarajiwa kwamba raia wa EAC watapata uelewa zaidi juu ya masuala mbalimbali ya mtangamano wa kanda na kujiona kuwa ni mali yao.

Mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa rasmi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afrika Masharikiwa, Biashara na Utalii wa Kenya, Phyllis Chepkosgey Kandie. Kauli mbiu ya mkutano huo ni ‘Afrika Mashariki tunayotaka.’ Zaidi ya wajumbe 100 wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo.