Breaking Newzzzz; Rostam kujivua gamba leo Igunga

MBUNGE wa Igunga, Rostam Azziz leo huenda akatangaza maamuzi magumu kwa kujivua gamba kuendelea na siasa jimboni kwake Igunga mkoani Tabora.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka kwa wadau wake wa karibu ambazo mtandao huu umezinasa mbunge huyo leo anatarajia kujiuzulu masuala ya siasa, jambo ambalo lilikuwa likizaniwa haliwezi kutokea.

Taarifa zaidi zinasema Rostam leo amewaita baadhi ya wahariri wakuu wa vyombo vya habari na amewasafirisha kwenda mkoani Tabora sehemu ambayo anakwenda kutangaza uamuzi huo ambao utakuwa mgumu.

Mbunge huyo pamoja na wenzake wawili yaani Andrew Chenge na Edward Lowassa wamekuwa wakituhumiwa kwa kashfa mbalimbali ndani ya Serikali na CCM jambo ambalo limewapa wakati mgumu hadi sasa. Wachambuzi wa masuala ya siasa walikuwa wakishauri watu hao kuanza kujivua gamba kwa kuondoka CCM, jambo ambalo limekuwa gumu hadi leo.
Mtandao huu unafuatilia zaidi na utakujuza kinachoendelea mara baada ya kupata taarifa zaidi kuhusiasa na kikao cha Rostam na baadhi ya wahariri wa kuu wa vyombo vya habari.