Dalili 6 Zinazopelekea Mwanamke Kufikiria Kuchit!

20130929-213938.jpg

Kwa mujibu wa Jarida maarufu la MensHealth, kuwa makini na sababu vyanzo vifuatavyo, ambavyo vinaweza kupelekea mke au mpenzio kutoka nje, yaani “Kuchit”.

1. Anatimiza miaka 20, 25, 30, 35…….miaka hii yenye kupishana Tano Tano ni hatari sana kwa Mwanamke, kwani ni nyakati ambazo anaanza kufikiria amefanya nini miaka mitano iliyopita? Atafikiria kwa kina kuhusu maisha yake katika suala zima la mapenzi, na kama hayaendi kama atakavyo, anaweza akatumia fursa ya Kuchit na jamaa mwingine kama njia ya kurekebisha mambo au kujifurahisha nafsi tu! Anasema Don-David Lusterman, PHD. Matukio ya wanawake wasio kwenye mahusiano ya furaha Kuchit yanaongezeka zaidi ya maradufu inapofika siku za sherehe zao za kuzaliwa.

Mwanaume anatakiwa afanye nini basi, ili kuepusha hili janga?: unatakiwa usicheze mbali na sherehe za kuzaliwa za mpenzi wako na sherehe za mwaka mpya, kwani hizi ndio siku ambazo Mwanamke anataka kuwa na mpenzi wake kitandani kuliko siku nyingine zozote.

2. Amepandishwa cheo kazini. Wanawake hupenda kujiwekea mipango na malengo, na wanapofikia malengo hayo- huenda wakajiuliza sasa nini kinafuata? Kama wapo kwenye uhusiano wenye misukosuko, basi ile konfidensi ya mafanikio waliyoyapata kazini inaweza ikapelekea wao kutafuta mahusiano bora zaidi, na hapo ndipo suala la Kuchit huanzia. Pia wanawake wenye mishahara minono wana asilimia kubwa sana ya Kuchit. Uchunguzi uliofanywa na Chuo Kikuu cha Washington uligundua kwamba wanawake wanaotengeneza $75,000 au zaidi kwa mwaka wana nafasi ya Kuchit mara 1.5 zaidi ya wale wanaotengeneza $30,000 kwa mwaka.

Mwanaume anatakiwa afanye nini, ili kuepusha hili janga?: sheherekea na jisikie ufahari kwa mafanikio ya mpenzio, kwani akiona hivyo atajisikia unamjali kama wanavyomjali kazini, hivyo basi hatokuwa na haja ya Kwenda kwa jamaa mwingine kutimiziwa matakwa ya nafsi (emotional support for her accomplishment).

3. Anahamia kuishi nyumba moja na wewe (maalum kwa wale ambao hawajaoana na wanaishi nyumba tofauti). Huenda ilikuwa ni wazo lake ku “move in” na wote mmefurahi, lakini tatizo sasa ni kwamba kutokana na kuwepo kwenu pamoja 24-7, na kushirikiana katika Kila maishani, kunakuwa hamna haja ya kuwa na mazungumzo marefu Kila mara. Hali hii inaweza ikatafsiriwa na Mwanamke kwamba sasa unamuona anaboa, yaani kwa ung’eng’e “boring”. Hivyo basi, inaweza ikapelekea yeye Kwenda nje na kutafuta mtu ambaye “bado anamuona yeye ana mvuto na aboi”, anasema Prof. Stuart Fischoff, wa Chuo Kikuu cha California, Los Angeles. Kwa uchunguzi uliofanywa na Jarida la MensHealth, umegundua kwamba asilimia 41 ya wanawake wanaochit hufanya hivyo na wafanyakazi wenzao.

Hapa pia tatizo huchangiwa na ile hulka ya “mipango na malengo”, ambayo wanawake wanayo kama tulivyogusia hapo mwanzo. Ni kwamba sasa Mwanamke ameshahamia kwako na mnaishi pamoja, kwa mawazo yake kinachofuatia ni ndoa na watoto……sasa kama mwanaume haweki hilo wazi, basi atarajie janga! Mtaalam mwingine wa mapenzi, Susan Heitler, aliyeandika kitabu kiitwacho “Power of Two”, anaongezea kwa kusema “lazima tukubali kwamba wanawake wengi wanataka kuolewa na kuwa na watoto, kwahiyo kama unawabania mojawapo au yote, basi jua kwamba una karibisha hatari ya Mwanamke Kwenda kwa jamaa mwingine, ambaye anaweza akampa hivyo vitu”

Mwanaume anatakiwa afanye nini, ili kuepusha hili janga?: weka wazi kwamba unafikiria kutumia fursa hii ya kuishi pamoja kama mwanzo wa mipango mikubwa ya baadae, yaani ndoa na watoto.

4. Anahisi mwanaume wake amechit. Matembezi ya visasi (revenge affairs) ni ya kawaida katika ulimwengu wetu wa leo. Mwanamke pia huamua kufanya matembezi au tembezi la kisasi katika jitihada za kurudisha hali ya kujisikia kwamba bado na yeye anahitajika, baada ya kuhisi au kugundua kwamba mwanaume wake anachit. Mtaalam Heitler anasema hapa kwamba hii ni hulka ya binaadam kwamba tunapenda kulipiza, kwahiyo Mwanamke akihisi ametendewa, basi nae huenda asiende nje kutafuta, lakini kama jamaa anajitokeza na kuchombeza, anakuwa mrahisi kukubali kutokana na kuwa na hasira za malipizi!

Kwa wale wanaume ambao hamchit, na bado Mwanamke wako haishi kukuhisi, basi huenda una Mwanamke mwenye kutojiamini (low confidence). Hivyo basi, mnashauriwa kutoa compliment za mara kwa mara kutoka moyoni, ili kutuliza nyoyo zao. Na kama mwanaume umechit, basi omba msamaha haraka iwezekanavyo na muonyeshe kwamba hautorudia tena, kama unataka usiwe mhanga wa hasira malipizi!

5. Hapati haki ya unyumba ipasavyo: oxytocin ni homoni(hormone) ambayo inauwezo mkubwa katika kukamilisha matakwa yetu ya kuwa karibu (bonding), yaani kuleta mahaba na ukaribu katika mapenzi. Hii homoni (oxytocin) huongezeka kiwango zaidi ya mara tatu au tano muda machache tu kabla ya kufika kileleni (orgasm). Kwa mijubu wa wataalam, hii homoni ina nguvu zaidi kwa wanawake kuliko wanaume. Kwahiyo basi, wanawake wanatengeneza ukaribu (bonding) zaidi kupitia kujamiiana (sex).

Kama haki ya unyumba haipatikani kama ilivyokuwa siku za mwanzo, basi anaweza akatafsri kama hapendwi tena, na hivyo Kwenda nje kutafuta ampendaye.

6. Amechoka na mahusiano, na yupo tayari kusonga mbele. Hii ni dalili au sababu ya mwisho, ambayo hutumiwa sana, sio tu na Wanawake, bali wanaume pia. David Buss, PHD., Profesa wa Saikolojia kutoka Chuo cha Texas, pale Austin na muandishi wa kitabu kiitwacho “The Evolution of Desire” aliwauliza wanaume 100 na wanawake, ni mbinu gani wanaweza wakatumia kumaliza mahusiano mabovu ya kimapenzi? Moja Kati ya majibu mengi aliyo pasta ni : kuanza mahusiano ya nje, yaani chit!!

Je Mwanaume au Mwanamke unaweza ukafanyaje kuepukana na janga hili?: hamna la kufanya zaidi ya kumuacha aende tu, kwani mpenzi anayetumia njia ya kuchit kama mbinu ya kumaliza mahusiano, hafai.

Mwisho……

Chanzo: Mean’s Health

Tafsiri: www.thehabari.com