Mashambulizi Katika “mall” ya Westgate Nchini Kenya Yalivyotokea

jinsi-mashambulizi-yalivyotokea-mall-westgate-nairobi-kenya-Al shabaab

  1. Washambulizi wa al shabaab waliingia kwenye mall ya Westgate kupitia milango ya mbele na gorofa ya pili wakitokea kwenye sehemu ya kupaki magari, punde tu baada ya kuingia wakaanza kurusha mabomu na kufyatua risasi. Maelfu ya raia wa kawaida wakaanza kukimbia kujaribu kuokoa maisha yao, Inasemekana kuwa Al shabaab walikuwa wanatafuta zaidi watu ambao sio Waislam. Wakachukua baadhi ya watu mateka na kuwashikilia kwenye ukumbi wa sinema na kasino.
  2. Baada kama ya saa moja hivi baada ya mashambulizi kuanza, polisi na majeshi ya Kenya yakawasili kwenye eneo la tukio, ndio Al shabaab na polisi wakaanza kurushiana risasi, majeshi yakaleta helcopter ili kuwasaidia katika opereshini hiyo, risasi zikaendelea kusikika usiku mzima.
  3. Ilipofika Jumapili, kati ya washambuliaji 10-15 wa Al shabaab walikuwa bado wapo ndani ya mall, mashambulizi yakaendelea siku nzima.
  4. Majeshi ya ulinzi ya Kenya wakaanzisha mashambulizi mapya, risasi zikaendelea kusikika, washambuliji wa Al shabaab walikuwa wanachoma magodoro na moshi mkubwa ulikuwa unaonekana juu ya jengo la mall. Ilipofika Jumanne jioni, Raisi Uhuru Kenyatta akatangaza kuwa wamefanikiwa kutuliza mashambulizi, watu waliokufa kwenye sakata hiyo ni 62 na inahisiwa  kuwa Kenya imepoteza wanajeshi 6.

Angalia Picha za Mashambuliza Katika Mall yalivyotokea Nairobi, Kenya