Na Magreth Kinabo- Maelezo
MTANZANIA anayedaiwa kuwatunza raia watano kutoka Nigeria wanaoishi nchini bila kibali halali na kumzuia Ofisa wa Uhamiaji kufanya kazi amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu.
Mshitakiwa huyo Mtanzania Chritopher Kanyala mwenye umri wa miaka 35 alipandishwa kizimbani, mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi wa mahakama hiyo, Warialwande Lema baada ya kutenda kosa kumzuia Ofisa Uhamiaji, Peter Bally wa Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam Septemba 17, mwaka huu.
Kanyala alidaiwa na Mwendesha Mashtaka, ambaye ni Ofisa Uhamiaji wa Mahakama ya Kisutu, Namtera Simba kosa hilo, ambapo alikana.
Akiendesha kesi hiyo, Hakimu huyo alisema upelelezi umeshakamilika na Mshatakiwa yuko nje kwa dhamana ya Sh. milioni tano na wadhamani wawili wa kuaminika ambao wasio walimu. Hakimu Lema alisema kesi hiyo itasikilizwa Oktoba 3, mwaka huu. Mshitakiwa huyo alikosa wadhamini na alirudishwa rumande.