Serikali yaagiza Ununuzi wa Mahindi Safi na Bora

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge Mhe. William V. Lukuvi (MB) akikagua Soko la Kimatifa la Mahindi la Isunta katika Wilaya ya Nkasi akiwa kwenye mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea sehemu za Ununuzi na Uhifadhi Mahindi nchini.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge Mhe. William V. Lukuvi (MB) akikagua Soko la Kimatifa la Mahindi la Isunta katika Wilaya ya Nkasi akiwa kwenye mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea sehemu za Ununuzi na Uhifadhi Mahindi nchini.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge Mhe. William V. Lukuvi amewaeleza wakala wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kuzingatia ubora na usafi wa ununuzi wa mahindi kwani mahindi yanayonunuliwa na Serikali ni kwa ajili ya Chakula.

Alisema hayo jana wakati wa Ziara yake ya ukaguzi wa vituo vya Mahindi vya Mtenga, Namanyere na Kasu vilivyopo Katika Wilaya ya Nkasi alipokuwa akipokea taarifa ya Ununuzi wa Mahindi katika vituo hivyo. Waziri Lukuvi alisema “itakuwa sio vizuri kununua mahindi ambayo yako chini ya kiwango na yaliyo na uchafu mwingi  kwakuwa Serikali inanunua mahindi kwa ajili ya matumizi ya chakula ni sivinginevyo, hivyo lazima Mahindi haya yawe masafi na yenge viwango bora  kwa walaji”.

“Mwaka huu Serikali imetoa bei nzuri ya Ununuzi wa Mahindi ya shilingi Mia Tano kwa kilo kwa kuzingatia uhitaji, kutokana na bei hiyo Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula NFRA inatakiwa kununua mahindi yaliyo safi ili kuweza kupanga viwango tofauti ambavyo vitawasaidia katika uuzaji wa Mahindi hayo kwa watu wengine. Kwa kupanga kupanga hovyo Wakala wa Hifadhi ya Chakula ya Taifa watapata wanunuzi wazuri, alisema Waziri Lukuvi”.

Alisisitiza kuwa kwa mwaka huu Serikali ndiyo mnunuzi mkubwa wa Mahindi katika Kanda zote Tanzania na Wakala wa Hifadhi ya Chakula ya NFRA ndiyo inayoongoza, katika ununuzi huo ambapo ameagiza NFRA kuanza haraka usafirishaji wa mahindi kwenda Mkoa wa Shinyanga mapema kabla kipindi cha mvua hakijaanza.

Akipokea taarifa ya ununuzi katika kituo cha Kasu, Waziri Lukuvi alielezwa kuwa kituo hicho kilipanga kununua Tani za Mahindi elfu 2000 hadi kufikia Mwezi Septemba,2013 hadi sasa kituo hicho kimeshanunua Tani 1,904 zenye thamani ya shilingi milioni 952,483,500 na kitaendelea na ununuzi hadi kufikia malengo ya Ununuzi wa Tani zilipangwa.

Akikamilisha ziara katika Mkoa wa Katavi, Waziri Lukuvi aliwapongeza wananchi wa Mkoa wa Katavi kwa jitihada zao za kilimo walizozionesha na kuwahakikishia kuwa katika kila msimu watalipwa fedha zao kwa wakati ili waweze kuendelea na kazi, pia ameielekeza NFRA kuhakikisha kuwa kila vibarua wanapomaliza kufanyakazi walipwe ili kupunguza madeni, NFRA ihakikishe kuwa kila vibarua wanapomaliza kazi zao walipwe mara moja wasisumbuliwe kwani fedha wanazopata zinawasaidia kuendesha maisha yao ya kila siku.