Kumbukumbu ya Mzee Shauri Timoth Nathan

Mzee Shauri Timoth Nathan  (18/08/1925-18/09/2007)

Mzee Shauri Timoth Nathan (18/08/1925-18/09/2007)

  

Sekunde, Dakika, Saa, Siku, Wiki, Mwezi, Mwaka na hatimaye mika mitano sasa imetimia tangu Mzee Shauri Timoth Nathan  (18/08/1925-18/09/2007) ututangulie Mbele za haki kama ulivyotutangulia kuja duniani Tarehe 18/09/2007 saa kumi na mbili jioni.
Nimajonzi
sana kwetu hasa ukizingatia kuwa uliondoka katika tarehe ambayo kitinda
mimba wako Mroki Mroki alizaliwa na ni siku kumi tu baada ya kufunga
ndoa Mroki “Father Kidevu”.
Unakumbukwa
na wengi sana maana ulikuwa ni mhimili mkuu katika familia, kipekee ni
Mke wako Mary O Nathan na watoto wako James Nathan, Mrs Stella Kaluse,
Lloyd Atenaka, Dossa Mroki,Freddrick (Kajiru) Mroki, Onesmo Nathan,
Thomas Nathan, Daniel Nathan, Kyaze Nathan, Namche Mroki, Kille Nathan
na Mroki Mroki na Wakwe zako wote.
Pia
unakumbukwa sana na Wajukuu zako Kidai Kaluse, Shauri Kaluse, Mfaume
Kilangi, Shauri James, Mwanaamani James, Hellena James, Nuru James,
Maria Kaluse, Ludao Kaluse, Kilave Atenaka, Maria Atenaka, Victoria
Dossa, Doureen Atenaka, Erick Mushi, Beatrice Mroki, Timothy Tomas,
Timothy Kajiru, Imanuel Kajiru, Eliewaha Kajiru, Timothy Kille, Maria
Thomas, Irine Atenaka, Anjela Chistian, Glory Mroki, Nathan Kyaze, Nathan
Dossa, Dinner Onesmo,Digna Onesmo, Debora Daniel na  Leonard Kyase
pamoja na Vitukuu wako pia kutoka kwa Mwanaamani, Kidai na Shauri.
Wananchi
na majirani zako wa pale Kijiji cha Kipera , Kitongoji cha
Kinyenze,Kata na Tarafa ya Mlali , Wilayani Mvomero mkoani Morogoro pia
wanakukumbuka sana pamoja na wote wa Ugweno, Kilimanjaro.
 
Tunakumbuka maneno yako ya Mwisho uliotuachia watoto wako kuwa “TUPENDANE, TUSAIDIANE na TUSHIRIKIANE,” baba hakika hili linatendeka na tupo na umoja uliotujengea na tunajivunia hilo.
Tunazidi kukuombea Baraka na pumziko jema maana sote uliotuacha tutakufata kama tulivyo kufuata hapa duniani.
Jina la Bwana Lihimidiwe Amina.