‘FFU’ ndani ya Internationals African Festival Germany


Bandi ya ‘FFU’ ikiwa jukwaani ikitumbwiza

*Jumamosi ya 16.07.2011 inakaribia
*Mabakuli ya “Supu ya Mawe” uwanjani kila moja na lake!

Bendi maarufu ya mziki wa dansi barani Ulaya “Ngoma Africa Band” aka FFU,kinatarajiwa kutumbuiza jukwaani tena katika onesho kubwa la aina yake African Internationals Festival, mjini Tübingen, ujerumani siku ya Jumamosi 16.Julai 2011.

FFU hao wa muziki pia wamepakua kutoka jikoni wimbo mpya uliobeba jina “SUPU YA MAWE” wimbo wenye ujumbe mahusus kwa walimwengu, ambao kwa sasa unasikika katika kambi ya FFU at ‘www.ngoma-africa.com’ wimbo huo ambao umetungwa na kamanda Ras Makunja akishirikiana na Christian Bakotessa aka Chris-B aka “Mshenzi” wa gitaa la solo.
Wimbo huo “Supu ya Mawe” ujumbe uliomo katika wimbo huo unaonekana kuwa na nguvu na vitamin zote za maisha kuliko kikombe cha dawa.
Kutokana na taarifa ya gazeti moja la kimataifa hili http://www.africa-news.eu/entertainment/44-entertainment/2815-welcome-to-international-african-festival-in-tubingen-germany.html bendi hiyo maarufu inazidi kupata umaarufu na kujizolea washabiki kiaina yake katika kila kona.
Usikose kuwasikiliza at www.ngoma-africa.com hili nawe upate bakuli la “Supu ya Mawe”
Soma habari zaidi:http://www.theafronews.eu/entertainment/welcome-to-international-african-festival-in-tubingen-germany