Muuaji Kambi ya Kijeshi US Atajwa

MTU ALIYEWAUA watu 12 katika kambi ya kijeshi nchini Marekani na kisha mwenyewe kuuawa, katika makabiliano na Polisi, ametajwa kuwa mwanajeshi wa zamaji wa jeshi la wanamaji.

Aaron Alexis, 34, kutoka Fort Worth, Texas, aliuawa na polisi baada ya kuvamia kambi hiyo na kuwaua watu kiholela , mjini Washington DC.

Taarifa zinazohusiana Marekani Watu wengine wanane walijeruhiwa kwenye uvamizi huo ulioanza mapema asubuhi mnamo Jumatatu.

Rais Barack Obama aliamuru bendera kupeperushwa nusu mlingoti katika Ikilu ya White House na Capitol Hill.

Alisema anaomboleza kwa sababu ya mauaji mengine ya halaiki na kulaani kitendo hicho cha uoga.

Haijulikani kwa nini Aaron Alexis aliamua kufanya shambulizi hilo na kuwaua watu kati ya umri wa miaka 46-73.

Awali polisi walichukua hatua baada ya ripoti za watu wengine kujihami wakishirikiana na Alexis, lakini baada ya msako mkali wakasema kuwa hakuna dalili kwamba Alexis alikuwa na wenzake..

Valerie Parlave wa shirika la ujasusi la FBI alisema kuwa Alexis, aliyekuwa ameajiriwa na mwanakandarasi aliyekuwa anafanya kazi kwenye mtandao wa internet wa FBI, alikuwa na pasi ya kuingia kwenye eneo hilo.

Na wakati huo huo watu wasiopungua 14 wameuawa kwa shambulio la risasi katika ukumbi wa cinema eneo la Aurora mjini Denver nchini Marekani.

Wakitoa taarifa hiyo polisi pia wanasema karibu watu 50 wamejeruhiwa katika shambulio hilo.

Walioshuhudia wanasema kuwa, mtu mwenye bunduki aliyevalia kinyago cha gasi usoni, alifyatua risasi usiku wa manane wakati onyesho la cinema ya The Dark Knight Rises likiendelea.

Mwanamume wa umri wa miaka 24 amekamatwa katika sehemu ya kuegesha magari ya ukumbi huo wa cinema akiwa na silaha mbili aina ya bunduki na bastola, huku polisi wakisema kuwa silaha zaidi zilikutwa katika ukumbi huo wa cinema.

Rais Barack Obama ameahidi kuhakikisha kuwa waliohusika katika shambulio hilo wanaletwa katika mkono wa sheria.

-BBC