Na Magreth Kinabo- Maelezo
CHAMA cha kutetea abiria Tanzania (CHAKUA) kimezishauri kampuni za usafirishaji zianzishe mfumo wa kukata tiketi kwa njia ya mtandao ili kuweza kuepusha usumbufu kwa abiria kutokana na wapiga debe, vishoka, wizi na tiketi feki kwa mabasi yaendayo mkoani.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari- MAELEZO kwa niaba ya Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa chama hicho, Modesti Mfilinge, mjumbe wa bodi hiyo, Renatus Kapira alisema uratibu huo utasaidia kupunguza tatizo la upandishaji nauli kiholela.
“Mfumo huo utasaidia kuwatambua kwa urahisi abiria wote waliokuwemo kwenye chombo husika pale inapotokea bahati mbaya wakapata ajali au au chombo kuharibika ili waweze kurudishiwa gharama na kulipwa fidia.
Chama hicho kimeishauri Serikali iangalie njia mbadala ya kuwasaidia abiria watakaokuwa wanatoka mbali kufuata vituo kwa mfano wanaotoka Mbagala,Kongowe au Chamanzi na maeneo mengine ya mbali kutuata basi la Arusha au Tanga, ambapo mtu mwenye familia hulazimika kutumia Sh. 50,000 hadi hadi Mbezi ya Kimara.
Aliongeza kuwa abiria wanaotoka maeneo hayo wanapata usumbufu kwa kuwa hakuna daladala zinatoka huko hadi katika kituo hicho. Kapira aliishauri Serikali kuwa iboreshe miundombinu katikavituo vya mabasi yanendayo mikoani ili kuwezesha abiria wanasubiri kusafiri kesho yake.
Aidha chama hicho kiliiomba Serikali kupitia vyombo vya usalama na mamlaka nyingine kufanya ukaguzi kwenye mabasi yanayosafirisha abiria mikoani kuwa ni si mabovu ili kuepusha ajali na usumbufu abiria.