Waziri Lukuvi kuanza ziara Mikoa ya Katavi, Rukwa na Mbeya
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Uratibu na Bunge), William V. Lukuvi (MB) anatarajia kuanza ziara yake rasmi katika Mikoa ya Katavi, Rukwa na Mbeya. Ziara hiyo inayoanza Septemba 16 hadi 19, 2013 inatarajia kutembelea miradi na shughuli anuai za maendeleo.
Katika ziara hiyo Waziri Lukuvi anatarajiwa kutembelea baadhi ya vituo vya Ununuzi wa Mahindi kwa ajili ya kuhifadhiwa kwenye Maghala ya National Food Reserve Agency (NFRA), Maghala ya NFRA ya kuhifadhi chakula, atapokea taarifa ya Utekelezaji kuhusu Mradi wa Miundo Mbinu ya Masoko na Uongezaji wa Thamani (MIVARF) katika maeneo yanayotekeleza mradi huu.
Vilevile Lukuvi atapokea Taarifa ya Utekelezaji wa Miradi yote ya Maendeleo ikiwemo Miradi itokanayo na ahadi za Mhe. Rais na Miradi itokanayo na Ilani ya Chama Tawala pamoja na Miradi inayofadhiliwa na Taasisi mbalimbali Mkoani humo.