Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Padri Joseph Monesmo Magamba, wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui, alipofika katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kumpa pole, Mjini Unguja, baada ya kumwagiwa tindikali na watu wasiojulikana katika Mtaa wa Mlandege Mkoa wa Mjini Magharibi jana jioni, Padri alimwagiwa Tindikali alipokuwa akitoka kupata huduma ya Mtandao.[Picha na Ramadhan Othman, Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Padri Joseph Monesmo Magamba wa
Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui, akitoa maelezo jinsi
alivyopata mkasa wa kutiwa Tindikali na watu wasiojulikanwa, katika mtaa wa Mlandege Mjini Unguja, alipofika katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kumpa pole, ambapo amelazwa na kuapatiwa matibabu.[Picha na Ramadhan Othman, Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akifafanua jambo wakati alipokuwa akiwafariji jamaa na wafuasi wa Padri Joseph Monesmo Magamba, wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui,waliofika kumuangalia Padri huyo
aliyelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja baada ya kumwagiwa
Tindikali na Watu wasiojulikana jana katika Mtaa wa Mlandege
Mjini Unguja. [Picha na Ramadhan Othman, Ikulu.]