Wakazi wa Iringa Waachana na Baridi Kushuhudia Serengeti Fiesta

Msanii maarufu kwa miondoko ya kipwani, Shilole, akitoa burudani kwa wakazi wa mjini Iringa na majirani zake katika tamasha la Serengeti Fiesta mjini hapo siku ya Jumapili katika uwanja wa Samora. Tamasha hilo linadhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti Kupitia bia yake ya Serengeti Premium Lager.

Mkurugenzi wa makampuni ya ASAS, Bw. Salim Abri Asas (kulia) akiwaonesha wanasemina (hawapo pichani) aina ya vitunguu alivyoamua kulima baada ya kuona bei yake katika moja ya maduka ya jumla (Supermarket). Asas aliahidi kusaidia shilingi milioni tano kwa watu wa Iringa waliohudhuria semina hiyo ili wafikirie watafanya nini, jumla ya vikundi sita viliundwa hapo hapo. NSSF pia wameahidi kuwapatia mafunzo na kuwaelimisha kuhusu faida ya kujiunga na NSSF. Pichani kushoto ni mmoja wa waratibu wa semina hiyo Bw. Simon Simalenga kutoka Clouds Media Group.

Mkurugenzi wa makampuni ya ASAS, Bw. Salim Abri Asas (kulia) akitoa elimu ya ujasiriamali kwa wanasemina (hawapo pichani) katika ukumbi wa St. Dominic mjini Iringa. Asas aliahidi kusaidia shilingi milioni tano kwa watu wa Iringa waliohudhuria semina hiyo ili wafikirie watafanya nini, jumla ya vikundi sita viliundwa hapo hapo. NSSF pia wameahidi kuwapatia mafunzo na kuwaelimisha kuhusu faida ya kujiunga na NSSF. Pichani kushoto ni mmoja wa waratibu wa semina hiyo Bw. Simon Simalenga kutoka Clouds Media Group.

MKOA wa Iringa unafahamika sana kwa miji yenye baridi kali kama vile Makambako, Ilolo na Mafinga siku ya jumapili maelfu ya wapenda burudani kutoka vitongoji hivyo mkoani Iringa walijitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Samora mjini humo kushuhudia katika Tamasha la Serengeti Fiesta.
Tamasha lilianza majira ya moja jioni kwa kutafuta mshindi wa Serengeti Fiesta supa nyota na wasanii wa kutoka Iringa na ilipotimu saa nne uwanja mzima ulilipuka kwa shangwe na furaha ambapo shoo ambayo wananchi wa Iringa walikuwa wakisubiri kwa hamu ilipoanza, Kwa jinsi baridi kali inavyokuwa majira ya jioni na usiku watu walisahau na kuachana na baridi hiyo kutokana na burudani waliyokuwa wakishuhudia kutoka kwa wasanii hao maarufu kama Shilole, Ney wa Mitego, Lina na wengine wengi.
Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa bia ya Serengeti Premium Lager ambayo ndio bia inayodhamini tamasha hili kubwa, Allan Chonjo alisema ”Mpaka sasa tumepata wawakilishi zaidi ya kumi na tano waliopata nafasi ya wageni maalum (VIP) kutoka mikoa ya Kigoma, Tabora Singida, Mtwara ambayo majina yao tumeshayatangaza, Mbeya na Iringa majina yao tutayatangaza rasmi mwisho wa wiki hii.
”Wawakilishi wote kutika mikoani watakaa jukwaa la watu maalumu ambapo wataweza kushuhudia burudani kwa karibu zaidi na watapata nafasi ya kupiga picha na wasanii wakubwa, hivyo tunawaomba wakazi wa Mtwara waendelee kunywa bia ya Serengeti ili waweze kujishindia bia za bure na hatimaye kushinda nafasi hiyo ya kuja Dar Es Salaam kwa ajili ya Fiesta ya mwisho”. Wateja wanatakiwa kuangalia chini ya kizibo na kuona kama wajishindia bia za bure, kwani kuna bia zaidi ya laki mbilli nchi nzima, aliongeza Chonjo.
Meneja wa bia ya Serengeti ambayo ndio bia inayodhamini tamasha hilo, Allan Chonjo, aliwashukuru na kukiri kwamba wakazi wa Iringa wamejitokeza kwa wingi sana na kwamba wanaburudika na bia ya Serengeti na vinywaji kutoka kampuni ya bia ya Serengeti kama ikiwamo bia ya Serengeti, Tusker Lager, Tusker Lite, Pilsner, Smirnoff Ice na nyingine nyingi kutoka kampuni hiyo.
“Watu wamekuwa wengi na tumejiandaa kwa kuwahudumia vinywaji kutoka kampuni yetu ya Serengeti, hivyo vinywaji vipo vya kutosha hatuna wasiwasi kwa hilo”. Alisema Chonjo.
Msanii Shilole ambaye alimpatia fursa ya kucheza naye jukwaani kijana mmoja mkazi wa Iringa alishangiliwa na uwanja mzima pale alipokuwa akicheza naye kwa mahaba. Naye mkali wa mahaba, Kassim Mganga pia alionyesha uwezo wake wa kuwaimbisha wapenzi hao kwa nyimbo zake za mahaba
Wasanii wengine kibao walifanya vizuri akiwamo Ney wa Mitego, Madee, Juma Nature, Shilole, Walter Chilambo, Stamina, Young Killer na Godzilla. Wengine ni Afande Sele, Ommy Dimpoz, Rich Mavoko, Chege, Temba, Kassim Mganga, Joh Makini na Nick wa Pili.