Rais Dk Shein Azinduwa Chuo cha Taaluma ya Sayansi na Afya

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, na Mshauri wa Mambo ya Afya, Wizara ya Afya ya Oman, Dk. Sayeed Sultan Bin Yarub Bin Qaatan Al- Busaid, wakikata utepe kama ishara ya ya uzinduzi wa jengo la madarasa ya Chuo cha Taaluma za
Sayansi ya Afya, lililogharamiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa ushirikiano na Serikali ya Oman, huko Mbweni  Nje ya Mji wa Unguja. [Picha na Ramadhan Othman, Ikulu.]

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akipokea risala ya Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya, kutoka kwa Mkuu wa Chuo hicho Dk. Haji Mwita, baada ya kuyazindua Rasmi madarasa ya Kusomea, yaliyojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Oman na ushirikiano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.[Picha na Ramadhan Othman, Ikulu.]

Mshauri wa Mambo ya Afya, Wizara ya Afya ya Oman, Dk. Sayeed Sultan Bin Yarub Bin Qaatan Al- Busaid, akitoa salamu zake wakati wa sherehe za uzinduzi wa madarasa mapya ya kusomea katika
Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya, yaliyojengwa na Serikali ya Oman, na ushirikiano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akitoa nasaha zake, baada ya kuyazindua rasmi madarasa ya chuo hicho, hapo chuoni Mbweni, Mkoa wa Mjini Mgharabi  Nje ya Mji wa Unguja, [Picha na Ramadhan Othman, Ikulu.]

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya, Dk. Haji Mwita, alipotembelea kuona vifaa mbali mbali vya kufundishia chuoni hapo alipofika kuzindua madarasa ya kusomea yaliyojenga kwa ufadhili wa Serikali ya Oman kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.[Picha na Ramadhan Othman, Ikulu.]