Meneja wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi (katikati) akichangia mada kwenye moja ya semina anuai zinazoendelea katika Tamasha la jinsia 2013 linalofanyika jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa marafiki wa TGNP kutoka nchini Kenya (aliye simama) akiwasilisha mada kwenye Tamasha la jinsia 2013 linalofanyika viwanja vya TGNP, Mabibo jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa Tamasha la Jinsia Tanzania 2013 linalofanyika viwanja vya TGNP, Mabibo jijini Dar es Salaam wakifuatilia mada anuai kwenye semina mbalimbali zinazowasilishwa kwenye tamasha hilo.
Kundi la watoto nalo lilipata fursa ya kufundishwa masuala mbalimbali katika tamasha hilo. Pichani ni mmoja wa wawasilishaji mada kutoka asasi ya Watoto Arts Organization -WAAO (aliyesimama kati ya watoto) akizungumza na watoto kwenye tamasha hilo.
Kundi la watoto nalo lilipata fursa ya kufundishwa masuala mbalimbali katika tamasha hilo. Pichani watoto wakiwa katika somo la vitendo namna ya kuandaa moja ya vyakula rahisi.
Kundi la watoto nalo lilipata fursa ya kufundishwa masuala mbalimbali katika tamasha hilo. Pichani watoto wakipata mafunzo kwa mmoja wa wawasilishaji mada kutoka TGNP (aliyesimama kushoto).
Moja ya kikundi cha sanaa kikifanya igizo kuonesha wanatamasha uzembe wa wafanyakazi katika taasisi za umma anuai muhimu nchini zinazogusa maisha ya kila siku ya Wananchi kihuduma.
Baadhi ya wawasilishaji mada wakizungumza na wana semina katika tamasha la jinsia linaloendelea jijini Dar es Salaam.
Picha mbalimbali juu ni warsha mbalimbali zikifanyika kwenye mkutano wa Tamasha la Jinsia Tanzania 2013 linalofanyika viwanja vya TGNP, Mabibo jijini Dar es Salaam.
Maonesho ya bidhaa anuai zinazotengenezwa na vikundi vya wajasiriamali
Maonesho ya bidhaa anuai zinazotengenezwa na vikundi vya wajasiriamali
Mmoja wa washiriki wa Tamasha la Jinsia Tanzania 2013 (kulia) akiangalia moja ya bidhaa maalumu zinazouzwa na TGNP ndani ya banda la mtandao huo.