Wananchi Wakaribishwa Kuchangia Maoni ya Mipango Kazi ya OGP

Coat of Arms of Tanzania


TAARIFA KWA UMMA

MWALIKO KWA WADAU KUCHANGIA MAONI KATIKA ZOEZI LA SERIKALI
KUJITATHMINI (SELF ASSESSMENT) KATIKA UTEKELEZAJI WA
MPANGO WA UENDESHAJI SHUGHULI ZA SERIKALI KWA
UWAZI (OPEN GOVERNMENT PARTNERSHIP)

Mwaka 2011, Serikali ya Tanzania ilijiunga na Mpango wa Kimataifa wa Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa Uwazi (Open Government Partnership – OGP). Uamuzi huu wa kujiunga na Mpango wa OGP unalenga katika kuongeza juhudi za Serikali katika kuweka uwazi zaidi katika uendeshaji wa shughuli zake; kushirikisha wananchi katika upangaji na utekelezaji wa shughuli za Serikali; kuimarisha uwajibikaji katika utendaji wa Serikali; kuimarisha juhudi za kuzuia na kupambana na rushwa na kuweka umuhimu wa matumizi ya teknolojia na ubunifu.

Kwa kuanzia Serikali imeanza kutekeleza ahadi (commitments) zilizoainishwa katika Mpango Kazi wake katika sekta tatu za kipaumbele za huduma za Afya, Elimu na Maji. Serikali imetekeleza ahadi zilizoainishwa katika Mpango Kazi wake kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Julai, 2012 hadi Julai, 2013. Kwa mujibu wa matakwa ya Mpango wa OGP, Serikali kwa kushirikiana na Asasi za Kiraia (Civil Society Organizations) inatakiwa kufanya zoezi la tathmini (Self Assessment) kujua ni kwa kiwango gani ahadi zilizoainishwa zimetekelezwa.

Kwa hiyo wadau wote na wananchi kwa ujumla wanakaribishwa kuchangia maoni ya jinsi mipango kazi ya OGP ilivyotekelezwa kwa kujaza fomu iliyopo kwenye tovuti www.ega.go.tz/ogp.

Maoni hayo ni muhimu katika kufanikisha zoezi la Serikali la kujitathmini na pia katika kuboresha maandalizi ya Mpango Kazi utakaotekelezwa katika kipindi kinachofuata cha miaka miwili kuanzia 2014 – 2016. Maoni yawe yamewasilishwa kabla ya tarehe 18 Septemba, 2013.

OFISI YA RAIS, IKULU

UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
PRESIDENT’S OFFICE – STATE HOUSE

PRESS RELEASE
CALL FOR STAKEHOLDER VIEWS ON THE GOVERNMENT SELF ASSESSMENT EXERSICE ON IMPLEMENTATION OF OPEN
GOVERNMENT PARTNERSHIP

Year, 2011, the government of Tanzania joined the global initiative of Open Government Partnership that aims at promoting transparency, empowering citizens, fighting corruption and encouraging use of new technologies to improve governance.
The Government started implementing its OGP commitments which were translated to action plans. During Phase I of OGP implementation, commitments were directed to three priority sectors which include Health, Water and Education. Hence, the one year plans which were implemented from July, 2012 to July, 2013 focused on the above mentioned priority sectors.
In accordance with OGP Regulations, after implementation for the period of one year, the government in collaboration with the Civil Society Organizations is required to conduct a Self Assessment Exercise to determine how the Programme was implemented.
Therefore, citizens are cordially invited to contribute their views and opinions on how the OGP action plans were implemented. All comments are to be presented in the forms which are found in the website www.ega.go.tz/ogp.
The Public views are crucial to facilitate government self assessment exercise in OGP implementation. Also the views will be used for developing next OGP action plans to be implemented between 2014/15 and 2015/16.
The views should be submitted through the above referred website before 18th Sept, 2013.
PRESIDENT’S OFFICE, STATE HOUSE