Na Mwandishi Wetu
MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Naseeb Abdul, juzi alifunika katika tamasha la Kili Music Tour lililofanyika kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika Mjini Kigoma.
Katika tamasha hilo lililohudhuriwa na umati wa mashabiki, Diamond alifanya onyesho la aina yake na kuwafanya mashabiki kumshangilia kwa kupiga kelele.
Diamond ambaye alikuwa msanii wa mwisho kupanda kwenye jukwaa, aliwaita wasanii wenzake ambao ndio wenyeji wa Kigoma kama Recho, Mwasiti pamoja na Linex na kuimba wimbo wa Leka Dutigite na kuwaamsha mashabiki waliofurika Uwanjani hapo.
Wasanii wengine ambao walitumbuiza katika onyesho hilo lenye ujumbe wa ‘Kikwetu Kwetu’ ilikuwa ni pamoja na Lady Jaydee, Barnaba, Ben Pol, Izzo Bizness, Recho, Prof. J, Fid. Q, Roma, Mwasiti, Linex pamoja na Kala Jeremiah.