Mwilli wa marehemu Leonard Uisso ukiwa ndani ya Kanisa la KKKT tayari kwa misa ya kuuombea kabla ya kusafarishwa kuelekea Kilimanjaro kwa mazishi.
Mwili wa marehemu Leonard Uisso ukiwasili Kanisani la KKKT Sinza kuombewa, kulia ni mtoto wa kiume wa marehemu John Uisso.
Mtoto wa marehemu Uisso, Peter Uisso aliyebeba msalaba mbele akiongoza msafara wa kuingiza mwiuli wa babayake kanisani.
Mke wa marehemu Leonard Uisso, kulia aliyeshikiliwa akiwasili KKKT Sinza pamoja na wanafamilia kwa ajili ya maombezi ya marehemu mumewe
Mke na watoto wa kiume wa marehemu Uisso wakiwa kanisani
Kutoka kushoto ni mke na watoto wa marehemu Leonard Uisso wakiwa kanisani pamoija na ndugu wa karibu wa familia hiyo.
Mke wa marehemu akilia baada ya kutoa salamu za mwisho kanisani
Mmoja wa viongozi wa CCM Sinza akitoa salamu za rambirambi kwa wafiwa, marehemu Uisso ni Mjiumbe wa Halmashauri Kuu ya Kata ya CCM Sinza.
Ni manjozi na vilio kanisani. Mtoto wa kike wa marehe uisso Zenna Uisso (katikati) akilia kwa uchungu baada ya kutoa heshima za mwisho
Mmoja wa viongozi wa Chadema Sinza akimfariji mtoto wa marehemu, Peter Uisso kabla ya kuanza safari kuelekea Moshi kwa mazishi. Peter ni miongoni mwa viongozi wa Chadema Kata ya Sinza.
Mtoto mkubwa wa kiume wa marehemu, John Uisso akilia kwa uchungu na kufarijiwa baada ya kutoa heshima za mwisho kwa marehemu baba yake kanisani.
Mwili wa marehemu Uisso ukiingizwa kwenye gari tayari kusafirishwa kuelekea Kilimanjaro kwa mazishi.