RAIS Robert Mugabe wa Zimbabwe ameyaonya mataifa ya Marekani na Uingereza na kuzitaka ziondoe vikwazo dhidi ya nchi yake, ama sivyo Zimbabwe italipiza kisasi.
Alisema hatua zao ni sawa na kusimbuliwa, na alisema wakati utafika kwa Zimbabwe kuchukua hatua za kujibu. Rais Mugabe alisema hayo katika mazishi ya afisa wa jeshi la wanahewa.
Hivi karibuni viongozi wa SADC walipokutana nchini Malawi walisema vikwazo vyote dhidi ya Zimbabwe sasa vinafaa kuondolewa baada ya kuridhika na hali ya uchaguzi uliokuwa huru na wa amani uliofanyika juzi.
-BBC