Waziri Sitta amjibu Mbowe

Waziri Samuel Sitta

Dodoma

WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye pia ni Kaimu Kiongozi wa shughuli za Bunge, Samuel Sitta amesema, hamshangai Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe (CHADEMA) kuiponda Serikali ya CCM na kutaka ilaumiwe kwa kutoimarisha miundombinu vijijini, hali iliyosababisha vijana wengi kukimbilia mijini.

Alisema hoja hizo hazina ukweli wowote kwani Serikali ya CCM inajitahidi kwa kila hali kuhakikisha inaimarisha miundombinu vijijini ili vijana waweze kujiajiri huko huko badala ya kukimbilia mijini.

“Jambo hili litazamwe kwa upana, Serikali ya CCM imefanya mengi katika kuhakikisha vijana walioko vijijini wanabaki huko.”

Alisema kwa kuzingatia hilo Serikali kupitia wakala wa Umeme vijijini (REA) inapeleka umeme vijini ili kuhakikisha kunakuwa na miundombinu ya kutosha kwa vijana kufanya shughuli mbalimbali za kujitafutia kipato wakiwa huko huko vijijini.

Pia alisema kuwa Serikali imeanzisha mpango wa Kurasimisha Ardhi Vjijini (MKURABITA) kwa lengo la kuwafanya vijana hao kuendelea kubaki huko na kufanya shughuli mbalimbali hususan za kilimo.

“Simshangai Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni bwana Freeman Mbowe,ni lazima aseme hivyo,lakini ni lazima suala hili tuliangalie kwa upana wake,Serikali imefanya mambo mengi ikiwa ni pamoja na kupeleka REA ili kupeleka umeme vijijini lakini pia imeanzisha MKURABITA haya yote ni kwa ajili ya kuwafanya vijana wawalioko vijijini wabaki huko na kufanaya shughuli za maenedeleo na kujitafuatia kipato badala ya kukimbilia mijini.”alisema Sitta na kuongeza

“Sikubali kwamba Serikali ya CCM ilaumiwe kwa hilo kwani imefanya mambo mengi kuhakikisha vijana wanabaki vijijini kufanya shughuli zao huko”

Katika swali la smsingi Mbunge wa Viti Maalum dKT.Mary Mwanjelwa alitaka kujua mpango wa Serikali wa kurejesha maeneo ya wazi ambayo yamekuwa yakigawiwa watu bila kuzingatia Mipangomiji husika lakini pia alitaka kujua hatua zilizochukuliwa dhidi ya watendaji waliogawa na mpaka sasa wanaendelea kugawa maeneo hayo kinyume cha sheria ,wakiwemo majaji na mahakimu na waliohalalishwa uuzaji wa maeneo hayo.

Akijibu swali hilo Niabu Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi Goodluck Ole-Medeye aliliambia Bunge kuwa Serikali ilishaanza mkakati wa kuyarejesha maeneo ya wazi yaliyovamiwa kwa ajili ya matumizi mengine kwenye Halmashauri za Miji na Wilaya.

Pia alisema kuwa Serikali huwachukulia hatua watumishi ambao hubainika kuwa walishiriki katika kugawa maeneo ya wazi kwa matumizi mengine ambapo hatua hizo ni pamoja na kuwaachisha kazi ,kuwashitaki mahakamani na kuwafungia leseni za kufanya kazi za kitaaluma.

Akitolea mfano wa hatu azilizokwishachukuliwa kwa waliobainika,Ole-Medeye alisema kuwa ,Juni 28 mwaka huu, watumishi sita walifikishwa mahakamani wakituhumiwa kuhusika na kugushi nyaraka na kugawa maeneo yaliyohifadhiwa kwa ajili ya matumizi ya Umma.