Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwenda viwanja vya Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma leo kuzindua Baraza la Ushauri la Viongozi wastaafu wa CCM. nyuma ya Kinana ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba.
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), wakishangilia wakati wa hafla ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kuzindua Baraza hilo
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimakribisha Rais Kikwete kuzindua Baraza la Ushauri la Viongozi wastaafu wa CCM leo mjini Dodoma. Wengine kushoto ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM (Bara) John Malecela, Mwenyekiti mstaafu wa CCM Rais Mstaafu Ali Hassan Miwnyi na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Dk. Ali Mohamed Shein na Kutoka kulia (walioketi) ni Makamu Mwenyekitin wa CCM mstaafu (Bara) Pius Msekwa, Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM (Zanzibar), Dk. Amani Abeid Karume na Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akizindua Baraza la Ushauri la viongozi wastaafu wa CCM, leo mjini Dodoma, huku akiwa na wajumbe wa baraza hilo na Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa CCM(Zanzibar) Dk. Ali Mohamed Shein.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akizungumza kabla ya kuzindua baraza hilo
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete ana Makamu wake (Zanzibar) Dk. Ali Moahammed Shein wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la ushauri la viongozi wastaafu wa CCM, baada ya kuzindua baraza hilo leo mjini Dodoma. Kushoto ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda na kulia ni Kinana.
Mwenyekiti wa Baraza la Ushsuri la Viongozi wastaafu wa CCM, Mwenyekiti mstaafu wa CCM na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi akiongoza kikao cha kwanza cha Baraza hilo leo mjini Dodoma. Kushoto ni Wajumbe wa Baraza hilo John Malecela na Amani Abeid Karume na kulia ni Mjumbe wa Baraza hilo, Benjamin Mkapa na Katibu wa Baraza Pius Msekwa.
Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao chca NEC kilichofanyika leo mjini Dodoma kama Baraza la Kitaifa la Kitaasisi kujadili maoni ya rasimu ya katiba mpya yaliyotolewa na mabaraza ya chini ya kitaasisi ya CCM hivu karibuni. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Dk. Ali Mohamed Sheni na kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Baadhi ya wajumbe wa NEC wakiwa kwenye kikao hicho
Wajumbe wa Baraza la Ushauri la viongozi wastaafu wa CCM, Kutoka kulia, John Malecela, Amani Abeid Karume na Pius Msekwa wakiwa kwenye kikao cha NEC, baada ya Baraza hilo kualikwa kwa ajili ya kushiriki katika mjadala wa rasimu ya Katiba mpya kwa upande wa CCM kama taasisi.
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM, Dk. Asha-Rose Migiro akiwasilisha makusanyo ya maoni ya katiba kama yaliyotolewa na mabaraza ya ngazi za chini ya CCM kama taasisi, leo kwenye kikao hicho cha NEC.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akijadiliana mambo na watendaji wenzake katika Chama, nje ya ukumbi wa White House mjini Dodoma leo, kabla ya kuzinduliwa Baraza la Ushauri la Wastaafu wa CCM . Kutoka kulia ni Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Muhamed Seif Khatib, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba na Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Taifa, Abdallah Bulembo.
Karibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimshauri Jambo Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete wakati wa uzinduzi wa Baraza la ushsuri la Wastaafu wa CCM leo mjini Dodoma.
Baadhi ya viongozi waliohudhuria katika uzinduzi wa Baraza hilo
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akimsalimia mmoja wa wana-CCM waliohudhuria hafla ya kuzinduliwa Baraza la Washauri la Wastaafu wa CCM leo mjini Dodoma
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM, Sadifa Hamis akishauriana jambo na Katibu Mkuu wa Jumuia hiyo, Martine Shigela wakati wa kikao cha NEC mjini Dodoma
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera, Costansia Buhiye akiwa katika ukumbi wakati wa kikao cha NEC leo mjini Dodoma.
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) leo kimedhihirisha kuwa ni chama imara na cha mfano duniani baada ya kuanzisha rasmi Baraza la Ushauri la Wazee wa CCM. Baraza hilo la aina yake linaundwa na Wenyeviti na Makamu wastaafu wa Chama, linategemewa kuwa nguzo bora katika kuimarisha chama. Chama Cha Mapinduzi ni chama pekee cha siasa nchi kutambua mchango wa wazee na kuwapa nafasi ya kuwa washauri wa chama.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa baraza hilo, Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema ‘Wazee hawa wamepitia vipindi muhimu vya uongozi katika nchi hii, akizungumzia Rais wa awamu ya Pili, alisema Mzee Mwinyi amebadilisha mfumo kutoka wa dola mpaka wa Soko, ametutoa kwenye mfumo wa chama Kimoja mpaka vyama vingi, ingawa Mzee mwinyi hakupata nafasi ya kuishi Maisha ya Vyama vingi, Mzee Mkapa amepokea taifa kwenye mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi.
Mzee Mwinyi alipokea nchi kwenye wakati mgumu sana, usafiri ulikuwa, kila kitu kilikuwa tabu bila kuuliza pesa umetoa wapi akasema ruksa. Mzee mkapa ameshujaisha mageuzi amepokea nchi ikiwa ndio imeingia kwenye mfumo wa vyama vingi na mageuzi makubwa ya mifumo ya kiuchumi.
Mwenyekiti wa CCM Taifa, akasema alivyokuwa kwenye mkutano wa SADC hivi karibuni kuna mtu alitoa maana ya neno retire..’maana yake sio kupumzika ila unaweka matairi mapya’
Kwa hatua hii Chama Cha Mapinduzi kimekamilika katika kila Idara na kimeonyesha kuwa wapinzani watachukua muda sana kufikia mafanikio haya maana wazee ni watu wenye heshima, uzoefu na busara nyingi katika kushauri na kufanya maamuzi hivyo kwa kuanzisha Baraza la Wazee, Chama cha Mapinduzi kitakuwa mfano wa kuigwa Africa na Dunia nzima.
Baraza hilo lenye kuwa na Marais wastaafu limebarikiwa kushiriki kikao cha kujadili rasimu ya katiba cha halmashauri kuu ya CCM Taifa. Baraza hilo ambalo mwenyekiti wake ni Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi na Katibu wake ni Spika Mstaafu Pius Msekwa pia lina wajumbe wengine akiwemo Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na Rais Mstaafu wa Zanzibar Salmin Amour.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na Waandishi wa habari leo mjini Dodoma kuhusu yaliyojiri katika kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichofanyika jana. Pamoja na mambo mengine, Nape amesema, Kamati Kuu amejadili suala ya sakata la madiwani wanane katika Halmashausri ya Bukoba, mkoani Kagera ambao Halmashauri Kuu ya CCM mkoa huo ilutangaza kuwatimua hivi karibuni ambapo Nape amesema, Kamati Kuu imeamua kuwaita ili kukutana nao kesho viongozi wanane katika mloa huo aliowataja kuwa Mwenyekiti na Karibu wa CCM mkoa wa Kagera, Mwenyekiti na Katibu wa CCM wilaya ya Bukoba mjini, Mbunge wa Bukoba mjini na Meya wa Halmashauri ya Bukoba.
IMETAYARISHWA NA BASHIR NKOROMO.